Dk. John Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) (Picha kubwa) na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe
Dk. John Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) (Picha kubwa) na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe

Mbowe amchongea Magufuli kwa wananchi

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amewataka watanzania kutokuogopa kumkosoa Rais John Magufuli pale anapokosea, anaandika Hellen Sisya.

Mbowe ameyasema hayo mapema leo hii katika hoteli ya Protea iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa endapo taifa litakuwa na watu waoga, basi kuna uwezekano wa taifa hilo kutawaliwa na dikteta.

“Anapostahili pongezi tumpe pongezi, anapostahili lawama tumpe lawama bila kuogopa. Tukiwa taifa la watu waoga Mwalimu Nyerere alituasa tutatawaliwa na dikteta “ amesema Mbowe.

Aidha, Mbowe amesisitiza kuwa watanzania wanapaswa kutambua kuwa kauli za Rais Magufuli sio sheria za nchi.

“Rais apongezwe pale anapofanya jambo jema. Lakini afanye jambo jema kwa misingi ya katiba, sheria pamoja na mikataba ambayo tunaingia. Tusiwe wepesi kumshangilia Rais kwa kila analolizungumza tukidhani ni jambo jema,” amesisitiza Mbowe

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn
FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amewataka watanzania kutokuogopa kumkosoa Rais John Magufuli pale anapokosea, anaandika Hellen Sisya. Mbowe ameyasema hayo mapema leo hii katika hoteli ya Protea iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa endapo taifa litakuwa na watu waoga, basi kuna uwezekano wa taifa hilo kutawaliwa na dikteta. “Anapostahili pongezi tumpe pongezi, anapostahili lawama tumpe lawama bila kuogopa. Tukiwa taifa la watu waoga Mwalimu Nyerere alituasa tutatawaliwa na dikteta “ amesema Mbowe. Aidha, Mbowe amesisitiza kuwa watanzania wanapaswa kutambua kuwa kauli za Rais Magufuli sio sheria za nchi. “Rais apongezwe pale anapofanya jambo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Hellen Sisya

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube