Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akipandiswa kwenye Ambulance kwa ajili ya kuelekea Airport kwenda Dar Es Salaam kwa Matibabu Zaidi.

Mbowe ahamishiwa Hospitali ya Aga Khani Dar

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni nchini Tanzania amehamishiwa Hospitali ya Aga Khani, Dar es Salaam kwa matibabu zaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mbowe alikuwa amelazwa Hospitali binafsi jijini Dodoma baada ya kudaiwa kushambuliwa na watu wasiojulikana katika makazi yake Area D jijini humo usiku wa kuamkia leo Jumanne tarehe 9 Juni 2020.

Mapema leo asubuhi, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika aliueleza umma wa Watanzania kwamba wanafanya mpango wa kumhamishiwa Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Leo jioni, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene ametoa taarifa akisema,”Mwenyekiti wa Chama Taifa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Mhe. Freeman Mbowe (Mb), amepokelewa muda mfupi uliopita Kitengo cha dharura Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi wa matibabu zaidi.”

Endelea kufuatilia MwanaHalisi Online & TV kwa habari zaidi

FREEMAN Mbowe, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni nchini Tanzania amehamishiwa Hospitali ya Aga Khani, Dar es Salaam kwa matibabu zaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu...(endelea) Mbowe alikuwa amelazwa Hospitali binafsi jijini Dodoma baada ya kudaiwa kushambuliwa na watu wasiojulikana katika makazi yake Area D jijini humo usiku wa kuamkia leo Jumanne tarehe 9 Juni 2020. Mapema leo asubuhi, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika aliueleza umma wa Watanzania kwamba wanafanya mpango wa kumhamishiwa Dar es Salaam kwa matibabu zaidi. Leo jioni, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene ametoa taarifa akisema,"Mwenyekiti wa Chama Taifa na Kiongozi…

Review Overview

User Rating: 4.05 ( 1 votes)

About Mwandishi Wetu

One comment

  1. Kwani Muhimbili hakuna wataalamu wa kutosha? Kwanini AgaKhan

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!