Bondia Floyd Mayweather akimrushia konde Manny Pacquaio

Mayweather hakuna ubishi tena, amtwanga kwa pointi Pacquiao

BONDIA Floyd Mayweather amekata ngebe za Mfilipino, Manny Pacquiao baada ya kumpiga kwa pointi na kutimiza kucheza mpambano wake wa 48 bila kupoteza.

Katika pambano la raundi 12, lililofanyika ukumbi wa MGM Grand jijini Las Vegas, Mmarekani huyo ameshinda kwa pointi za majaji wote, 118-110, 116-112 na 116-112.

Mayweather sasa ni bingwa wa dunia asiyepingika katika uzito wa Welter na mmiliki wa mataji yote makubwa, WBA, WBO na WBA.

Tofauti na ilivyotarajiwa, Pacquiao hakuweza kurusha ngumi nyingi kutokana na mpinzani wake kuhama hama ulingoni.

Mayweather aliitumia vizuri staili yake ya kupigana kwenye kona na kufanikiwa kumtupia ngumi nyingi za kudonoa mpinzani wake kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Kufika raundi ya 11, tayari mwelekeo wa pambano ulianza kuonekana ‘Mtu Pesa’ atashinda ingawa Man Pac alikuwa anashangiliwa zaidi ukumbini.

Mayweather alistahili ushindi na alionyesha yeye ni bondia bora wa kizazi cha sasa.

BONDIA Floyd Mayweather amekata ngebe za Mfilipino, Manny Pacquiao baada ya kumpiga kwa pointi na kutimiza kucheza mpambano wake wa 48 bila kupoteza. Katika pambano la raundi 12, lililofanyika ukumbi wa MGM Grand jijini Las Vegas, Mmarekani huyo ameshinda kwa pointi za majaji wote, 118-110, 116-112 na 116-112. Mayweather sasa ni bingwa wa dunia asiyepingika katika uzito wa Welter na mmiliki wa mataji yote makubwa, WBA, WBO na WBA. Tofauti na ilivyotarajiwa, Pacquiao hakuweza kurusha ngumi nyingi kutokana na mpinzani wake kuhama hama ulingoni. Mayweather aliitumia vizuri staili yake ya kupigana kwenye kona na kufanikiwa kumtupia ngumi nyingi za kudonoa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Masalu Erasto

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram