Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mawaziri wapya 21, waliotemwa hawa hapa
Habari za SiasaTangulizi

Mawaziri wapya 21, waliotemwa hawa hapa

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mawaziri 21, Naibu Mawaziri 23 na wabunge wawili aliowateua kisha kuwapangia wizara za kuhudumu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Baraza hilo limetangazwa leo Jumamosi tarehe 5 Desemba 2020 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi Ikuku ya Chamwino jijini Dodoma.

Mawaziri hao 21 wanaungana na wawili waliokwisha teuliwa na kuapisha na kufikisha idadi ya mawaziri 23.

Mawaziri hao waliokwisha teuliwa ni na kuapishwa ni; Dk. Philip Mpango (Fedha na Mipango) na Profesa Palamagamba Kabudi wa Mambo ya Nje.

Katika uteuzi huo, Rais Magufuli amewateua wabunge wawili wa Bunge la Tanzania, Dk. Doroth Gwajima na Dk. Leonard Chamriho ambao kwa pamoja amewateua pia, kuwa mawaziri.

Dk. Gwajima aliyekuwa naibu katibu mkuu Tamisemi, anayeshughulikia afya ameteuliwa kuwa waziri wa afya huku Dk. Chamriho akiteuliwa kuwa waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano.

Balozi John Kijazi

Rais Magufuli ameanzisha wizara moja ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari ambayo itaongozwa na Dk. Faustine Ndugulile.

Baraza hilo, limeshuhudia sura mpya na panga pangua huku Rais Magufuli aliwaacha baadhi ya mawaziri aliomaliza nao mhula wa kwanza wa utawala wake wa miaka mitano.

Baadhi ya mawaziri walioachwa waliohudumu hadi mwisho ya ungwe ya kwanza ya Rais Magufuli ambao wameachwa na wizara zao kwenye mabano ni; Dk. Hamis Kingwangala (Maliasili na Utalii), Luhaga Mpina (Mifugo na Uvuvi), Isack Kamwelwe (Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano) na Profesa Makame Mbarawa (Maji).

Dk. Damas Ndumbalo

Wengine ni; Mussa Zungu (Muungano na Mazingira) na Japhet Hasunga (Kilimo).

Baadhi ya Naibu Mawaziri walioachwa ni; Juliana Shonza (Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), Stella Manyanya (Viwanda na Biashara), Costantine Kanyasu (Maliasili na Utalii), Stanslaus Nyongo (Madini), Subra Mgalu (Nishati), Hamad Masauni (Mambo ya Ndani) na Dk. Ashatu Kijaji (Fedha na Mipango).

Mwigulu Nchemba, Waziri wa Katiba na Sheria

Waliotangazwa leo na wizara zao ni;

1. Elias Kwandikwa -Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
2. Jumaa Aweso- Maji
3. Kepteni mstaafu George Mkuchika – Utawala Bora
4. Wiliam Lukuvi- Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
5. Innocent Bashungwa – Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
6. Jenista Mhagama – Sera, Bunge, Ajira, kazi na Wenye Ulemavu
7. Profesa Kitila Mkumbo- Uwekezaji
8. Dk. Mwigulu Nchemba – Katiba na Sheria
9. Mashimba Ndaki – Mifungo na Uvuvi
10. Dk. Damas Ndumbaro – Maliasili na Utalii
11. Selemani Jaffo – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)
12. Dk. Medard Kamelani – Nishati
13. Profesa Adlof Mkenda- Kilimo
14. Doto Biteko – Madini
15. George Simbachawene – Mambo ya Ndani
16. Ummy Mwalimu – Muungano na Mazingira
17. Dk. Faustine Ndugulile – Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
18. Dk. Dorothy Gwajima – Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
19. Dk. Leonard Chamriho – Ujenzi na Uchukuzi
20. Geofrey Mwambe- Viwanda na Biashara
21. Profesa Joyce Ndalichako – Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Naibu mawaziri ni;

1. Kigahe Silaoneka- Viwanda na Biashara-
2. Angelina Mabula- Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi-
3. Ptrobas Katambi – Kazi, Vijana na Ajira
4. Hamis Hamza Hamis -Mambo ya Ndani
5. Mwanaidi Ali Hamis- Fedha na Mipango-
6. Kipanga Omary- Elimu Sayansi na Teknolojia-
7. Dk. Festo Lugange – Tamisemi
8. Stephen Byabato -Nishati
9 Ndejembi John- Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala bora-
10. Kundo Mathew -Mawasiliano na Telnolojia ya Habari
11. Pauline Gekul -Mifugo na Uvuvi
12. Ndulane Kumba – Madini
13. Msongwe Kasekenya – Ujenzi
14. Ummy Nderiananga – Wenye Ulemavu
15. Maryprisca Mahundi – Maji
16. Abdallah Ulega -Habari, Umaduni, Sanaa na Michezo
17. David Silinde- Tamisemi
18. Husein Bashe – Kilimo
19. Dk. Godwin Mollel -Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na watoto
20 Gefrey Pinda – Katiba na Sheria
21. Mwita Waitara – Muungano na Mazingira
22. William Ole Nasha – Mambo ya Nje
23. Mary Masanja – Maliasili na Utalii

Balozi Kijazi amesema, wateuliwa hao wataapishwa wiki ijayo.

6 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!