MAWAZIRI wanaohudumu kwenye utawala wa awamu ya tano chini ya Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli ‘wamekatwa’ kwenye mchakato wa kuwania ubunge ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Jana Alhamisi tarehe 20 Agosti 2020, Halmashauri Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake, Rais Magufuli ilihitimisha safari ya mwezi moja na nusu ya kupata wagombea ubunge wa majimbo na viti maalum.
Katika uteuzi uliofanywa na kikao hicho, ulionyesha wateule wa Rais Magufuli kwenye baraza lake, mawaziri wawili na naibu mawili wawili wameangukia pua.
Mawaziri kamili ni, Dk. Harisson Mwakyembe wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Angellah Kairuki wa Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji.
Pia, kuna naibu mawaziri, Omary Magumba wa Kilimo na Dk. Mary Mwanjelwa wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Dk. Makyembe ameshindwa kutetea nafasi yake ya ubunge Kyela Mkoa wa Mbeya ambapo aliyeteuliwa ni Ally Jumbe.
Waziri mwingine ni Angellah Kairuki wa Uwekezaji.
Kairuki alikuwa mbunge wa viti maalum ambaye katika mchakato wa uchaguzi mwaka huu, alikwenda kugombea jimbo la Same Magharibi.
Aliyeteuliwa ni Dk. Mathayo David ambaye aliongoza kura za kaoni katika harakati zake za kutetea jimbo hilo alilokuwa akiliongoza.
Omary Mgumba, naibu waziri wa kilimo, yeye ameshindwa kutetea nafasi yake jimbo la Morogoro Kusini Mashariki.
Safari ya Mgumba ilianza kuingia doa baada ya Hamis Shabani maarufu Babu Tale, Meneja wa mwanamuziki nchini Diamond Platinum kumshinda kura za maoni na hatimaye kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu.
Dk. Mary Mwanjelwa, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora aliyekuwa akiwanua viti maalum mkoa wa Mbeya, amejikuta akiangukia pua licha ya kuongoza katika kura za maoni.
Huyu wa Mbeya si inasemekana alikuwa akigawa bahasha za takrima kwa wajumbe wa CCM?
Da ! Kuna sehemu nyingine sasa viongozi wa ccm wamepewa kazi ngumu kupotishiwa wetu ambao hata hawajulikani na hii inawapa nafasi vyama vya upinzani
frankamos84@gmail.com