Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mawaziri Simbachawene, Ngonyani wang’oka, Prof. Mruma abebwa
Habari za SiasaTangulizi

Mawaziri Simbachawene, Ngonyani wang’oka, Prof. Mruma abebwa

George Simbachawene, aliyekuwa Waziri wa TAMISEMI. Picha ndogo Mhandisi Edwin Ngonyani, aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi
Spread the love

MAWAZIRI wawili wa serikali ya awamu ya tano, wameachia ngazi muda mfupi baada ya Rais John Magufuli kuwataka kufanya hivyo leo asubuhi, anaandika Irene David.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), pamoja Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Edwin Ngonyani wametangaza kuachia ngazi leo hii muda mfupi baada ya Rais Magufuli kumaliza kuhutubia.

Kujiuzulu huko kunatokana na agizo la Rais Magufuli ambalo amelitoa baada ya kukabidhiwa ripoti mbili za madini ya Tanzanite na Almas.

Kujiuzulu kwa Mawaziri hao kumeripotiwa moja ya Luninga muda mfupi bada ya Rais Magufuli kumaliza hotuba Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Kamati ya Bunge ilichunguza masuala mbalimbali katika sekta hiyo na kutoa ripoti kwa Spika Job Ndugai ambaye alikabidhi kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye leo na yeye amemkabidhi Rais Magufuli.

Akitoa hutuba baada ya kupokea ripoti hizo, Rais Magufuli aliagiza watendaji wa serikali waliotajwa katika ripoti kuachia ngazi mara moja kupisha uchunguzi.

“Kama ni Waziri, Katibu Mkuu, Mkurugenzi ama mtu yoyote aliyetajwa lazima atupishe ili uchunguzi uweze kufanyika,” amesema

Wenyeviti wa kamati hizo ni pamoja na Mbunge, Azzan Zungu na Dotto Biteko ambao jana walikabidhi ripoti hizo kwa Spika wa Bunge.

Aidha, Rais ameipongeza kamati hiyo kwa kufanya kazi kubwa ya kizalendo yenye kulisaidia taifa na kuibua madudu mengi ambayo yangeligharimu taifa na kusema kama tume hiyo ingekuwa ya juu juu angeikataa.

Rais amemshukuru pia Prof Mruma kwani alikuwa akifanya uchunguzi na kuibua siri zote zilizofichika katika sakata hili.

Katika ripoti ya Zungu, Mruma alionekana kuruhusu madini ya Almasi yapotee kwa kusaini bila kusoma nyaraka kwa kisingizio cha kuwaamini watendaji wa wizara.

Aidha, ripoti hiyo pia ilibaini Waziri Simbachawene amekutwa na hatia ya kusaini mikataba yenye madudu mengi yaliyoingiza nchi kwenye hasara kubwa.

Makada wengine wa CCM waliotajwa ni pamoja na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo.

Profesa Muhongo aliingia ofisini mwaka 2012 kwa mara ya kwanza kama Waziri wa Nishati na madini, lakini akasaini leseni za uchimbaji wa Tanzanite ‘retrospectively’.

Hata hivyo, Rais Magufuli amemuokoa Profesa Mruma kutoka mtego wa Kamati ya Bunge iliyochunguza biashara ya madini ya almasi hapa nchini na kusema kwamba msomi huyo alitumwa kama askari kwenda kufanya kazi maalum.

Profesa Mruma aliongoza Tume iliyoundwa na Rais Magufuli kuchunguza Makinikia ya dhahabu na kumpa ripoti miezi michache iliyopita na leo, amesema kutajwa katika ripoti hiyo ilikuwa ni lazima kwa sababu alikuwa ametumwa huko kwa makusudi kwenda kuchunguza wizi unaofanywa kwenye almasi.

Aidha, ameomba Spika kuandika barua kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhusu wabunge wake ambao wametajwa katika ripoti hiyo ili waweze kuchukua hatua zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!