Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mawakili wamuweka Zitto njia panda
Habari za Siasa

Mawakili wamuweka Zitto njia panda

Zitto Kabwe
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam inatarajia kuamua kupokea au kutopokea kielelezo cha upande wa mashitaka (Jamhuri). Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Ushahidi huo ni tepu ya CD, iliyowasilishwa mahakamani hapo kwenye kesi ya uchochezi inayomkabili Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Leo tarehe 3 Decemba 2019, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, mtalaamu wa uchunguzi wa picha kutoka Jeshi la Polisi E3234 Sajent James, akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumain Kweka akisaidiwa na Wakili Nassoro Katuga, amewasilisha CD hiyo, aliyodai alipewa aifanyie uchunguzi kama ni halisi na haijahaririwa.

Shahidi huyo amedai, aliletewa CD hiyo inayomuonesha Zitto kuichunguza kama haijahaririwa, amesema ni halisi na anajua picha ambazo zimehaririwa.

Sajent James ameeleza, picha ili uijue kuwa halisi, maneno ya mzungumzaji yanakwenda sambamba. Baada ya kueleza sifa hizo, ameiomba mahakama kupokea kielelezo hiko kitumike kama ushahidi.

Upande wa utetezi uliongozwa na wakili Jebra Kambole, akisaidiwa na Frank Mwakibolwa, umepinga mahakama hiyo kupokea kielelezo hiko kwa kuwa, huo ni ushahidi wa kieletroniki na kwa mujibu wa sheria ya ushahidi wa kieletroniki namba 18 ya mwaka 2015, kimeweka wazi kwa namna gani ushahidi wa aina hiyo unawasilishwa mahakamani.

Jebra ameeleza kuwa, hakuna ubishani kuwa CD hiyo imewasilishwa mahakamani hapo na mtu ambaye hakuhusika kwenye upigaji wa picha hiyo.

“Shahidi ameshindwa kukidhi vigezo vya kifungu cha 18 (c), lakini pia kwa kuwa sio yeye aliyepiga hiyo picha, ameshindwa kuelewa namna gani video hiyo imerekodiwa,” amesema.

Upande wa Jamhuri, Wakili Katuga akijibu hoja hizo ameeleza kuwa, ushahidi huo umefanyiwa uchunguzi na mtaalamu wa picha na kwamba, aliyepiga picha hiyo ni askari na aliyefanya uchunguzi ni askari mwenye utaalamu wa picha.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Hakimu Shaidi ameeleza kuwa atatoa uamuzi juu ya kupokelewa kwa kielelezo hicho kesho asubuhi tarehe 3 Desemba 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

error: Content is protected !!