Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mauaji Z’bar: IGP Sirro, Zitto wavutana
Habari za Siasa

Mauaji Z’bar: IGP Sirro, Zitto wavutana

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo
Spread the love

TAKWIMU za Jeshi la Polisi na Chama cha ACT – Wazalendo kuhusu mauaji yaliyotokea Zanzibar wakati wa uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, zinakinzana. Anaripoti Hamis  Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Wakati Jeshi la Polisi likisema, vifo hivyo vilikuwa viwili, Chama cha ACT – Wazalendo kilieleza kuwa vifo hivyo vilifika 13.

Katika ripoti ya ACT- Wazalendo iliyosomwa na Zitto Kabwe, kiongozi wa chama hicho tarehe 8 Novemba 2020 ilieleza, vifo hivyo vilikuwa 13, majeruhi 130 na watu waliokamatwa na Jeshi la Polisi 120.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 19 Novemba 2020, kuhusu takwimu za mauaji hayo, IGP Sirro amesema, si kweli kwa kuwa, watu waliopoteza maisha visiwani Zanzibar kutokana na vurugu za uchaguzi wawili tu.

“Madai watu wengi wamekufa Kaskazini na Kusini Pemba ni uongo, taarifa tulizonazo watu wawili wamefariki,  tarehe 26 mmoja alikufa siku ZEC (Tume ya Uchaguzi Zanzibar) wanatawanya vifaa vya kupigia kura na mwingine alikufa tarehe 27 Unguja sababu ya vurugu,” amesema IGP Sirro.

Amesema, mtu mmoja alipoteza maisha tarehe 26 Oktoba 2020 katika vurugu zilizofanywa na wafuasi wa upinzani waliokuwa wanazuia maofisa wa ZEC, kusambaza vifaa vya kupigia kura.

IGP, Simon Sirro

“Hii ilijitokea tarehe 26 Kaskazini Pemba ZEC wakisambaza vifaa vya kupigia kura, walishambuliwa watendaji wake na jeshi ilibidi iingilie kati kurudisha amani. Kuna baadhi ya askari waliumia, askari mmoja alipigwa risasi mguuni, waliohusika walikamatwa.

“Tarehe 27 ilipita vizuri lakini Kaskazini Pemba kwa wakereketwa wa upinzani ili kuwa shida,  walitaka uchaguzi usifanyike, wakaandamana kwenda kupiga kura. Unapigaje kura siku ya makundi maalumu?  Ilibidi tuwakamate na wengibe kuwafikisha mahakamani,” amesema IGP Sirro

Wakati huo huo, IGP Sirro amesema katika vurugu za uchaguzi huo, askari mmoja aliuawa kwa kuchinjwa na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa upinzani.

Amesema, tukio hilo lilitokea tarehe 28 Oktoba 2020 katika Mkoa wa Kusini Pemba, ambapo watuhumiwa baada ya kumteka askari huyo, walimpora silaha iliyokuwa na risasi 30.

“Kule Kusini Pemba tarehe 28 Oktoba 2020, askari wetu aliviziwa akakamatwa na wakereketwa naamini wa vyama vya upinzani, alichinjwa na baada ya kuchinja waliondoka na silaha yenye risasi 30. Kwa juhudi za polisi juzi tuliweza kukamata silaha ikiwa na risasi 21 kwa maana tisa zimetumika,” amesema IGP Sirro.

IGP Sirro amewataka wananchi wenye taarifa za ziada kuhusu idadi ya watu waliopoteza maisha visiwani humo kuzifikisha katika Jeshi la Polisi ili zifanyiwe kazi.

Amesema, Jeshi la Polisi likipata taarifa hizo zitakazoonesha majina ya marehemu na maeneo ambayo miili yao ilizikwa, litaomba kibali mahakamani ili lifukue maiti kwa ajili ya kuzifanyia uchunguzi wa chanzo cha vifo hivyo.

Pia IGP Sirro amezungumzia vurugu zinazodaiwa kufanywa na wanamgambo wenye itikadi kali ya kiislamu mkoani Mtwara maeneo ya mpakani mwa Tanzania na nchi ya Msumbiji, akisema kwamba watu kadhaa wamekamatwa kwa tuhuma hizo.

Amesema , miongoni mwa waliokamatwa ni raia wa Tanzania na kwamba, Jeshi la Polisi bado limeweka kambi katika maeneo hayo ili kuhakikisha usalama wa raia.

“Mtwara tuanendelea vizuri vyombo vya ulinzi viko vya kutosha, tukio lile kuna watu wetu wanahusika. Katika Kijiji cha  Kitaya kuna watu wanahusika. Watu wanakiri Watanzania wanahusika na matukio hayo, wanaoletwa kutoka Msumbiji wanawaonyesha njia,” amesema IGP Sirro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!