Mauaji ya watu 166 Ethiopia

Spread the love

JESHI la Polisi nchini Ethiopia, limethibitisha mauaji ya watu 166, raia wa taifa hilo kwenye maandamano ya kulaani mauaji ya mwanamuziki Haacaaluu Hundeessa. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

“Mauaji ya watu 166 yametokea kwenye maandamano yanayofanywa na waandamanaji kutokana na kifo cha Haacaaluu Hundeessa.

“Kutokana na kifo hicho, raia 145 na polisi 11 wamepoteza maisha. Jumla yake ni 166, wengine 10 wameuawa katika Jiji la Addis Ababa,” amefafanua Girma Gelam, Kaimu Mkuu wa Polisi katika Mji wa Oromia.

Girma amesema, watu 167 wana majeraha mabaya na kwamba watu 1,084 wamekamatwa na polisi kwa kujihusisha na maandamano hayo.

Haacaaluu ambaye ni mwanamuziki maarufu wa miondoko ya Pop, kutoka kabila kubwa kuliko yote nchini humo la Oromo, alipigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana usiku wa Jumatatu wiki iliyopita.

Mauaji hayo yameibua hisia za kikabila na kutishia mwendelezo wa demokrasia iliyoanza kuchipua. Mpaka sasa, watu watano wamekamatwa wakihusishwa na mauaji hayo.

JESHI la Polisi nchini Ethiopia, limethibitisha mauaji ya watu 166, raia wa taifa hilo kwenye maandamano ya kulaani mauaji ya mwanamuziki Haacaaluu Hundeessa. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea). “Mauaji ya watu 166 yametokea kwenye maandamano yanayofanywa na waandamanaji kutokana na kifo cha Haacaaluu Hundeessa. "Kutokana na kifo hicho, raia 145 na polisi 11 wamepoteza maisha. Jumla yake ni 166, wengine 10 wameuawa katika Jiji la Addis Ababa,” amefafanua Girma Gelam, Kaimu Mkuu wa Polisi katika Mji wa Oromia. Girma amesema, watu 167 wana majeraha mabaya na kwamba watu 1,084 wamekamatwa na polisi kwa kujihusisha na maandamano hayo. Haacaaluu ambaye ni mwanamuziki maarufu…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!