Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mauaji ya Ndadaye: Rais Burundi afungwa maisha
Kimataifa

Mauaji ya Ndadaye: Rais Burundi afungwa maisha

RAIS wa zamani wa Burundi, Pierre Buyoya
Spread the love

PIERRE Buyoya, Rais Mstaafu wa Burundi, amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada kubaini kuhusika katika mauaji ya aliyekuwa rais wa taifa hilo, Melchior Ndadaye. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Mahakama Kuu nchini humo, imeeleza kuridhika na ushahidi wote uliotolewa mahakamani na mazingira halisi ya Buyoya kuhusika katika mauaji ya Mdadaye mwaka 1993.

Mahakama imeeleza, Buyoya “alifanya shambulizi dhidi ya kiongozi wa taifa aliyekuwa madarakani” na hatimaye kumuua kiongozi wa kwanza aliyechaguliwa kwa njia ya demokrasia nchini humo.

Mauaji hayo ya uvamizi, yaliyofanywa na Buyoya, yaliitumbukiza Burundi kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Katika hukumu hiyo, maofisa 18 wa ngazi za juu wa jeshi wakati huo pamoja na watu waliokuwa karibu na kushirikiana na Buyoya, wamehukumiwa kifungo cha namna hiyo.

Taarifa kutoka Burundi na kuchapwa kwenye mitandao mbalimbali ya kimataifa zinaeleza, watu watatu waliokuwa wakihusishwa na mauaji hayo, wamefungwa miaka 20 jela.

Waziri Mkuu wa wakati huo, Antoine Nduwayo ameachwa huru.

Wakati wa hukumu hiyo, ni watuhumiwa watano tu ndio waliokuwepo huku wengine wakihukumiwa vifungo hivyo licha ya kutokuwepo mahakamani.

Baada ya Burundi kupata Uhuru wake 1962, taifa hilo liliingia kwenye sintofahamu kutokana na kabila kubwa la Wahutu na Watusi kuingia kwenye mgogoro wa madaraka.

Buyoya ambaye ni Mtusi, aliingia madarakani kama rais wa taifa hilo mwaka 1987 kwa njia ya mapinduzi. Kwenye uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia, Buyoya aliangushwa na Ndadaye (Muhutu) mwaka 1993.

Hata hivyo, Ndadaye aliuawa miezi mine tu baada ya kuingia Ikulu ya Burundi, alivamiwa na askari wa Kihutu wenye msimamo mkali.

Mauaji hayo yalisababisha vurugu za kikabila na kusababisha mauaji ya watu zaidi ya 300,000. Mauaji hayo yalikoma mwaka 2006.

Baada ya mauaji hayo, Buyoya alirejea madarakani na kuongoza taifa hilo kuanzia mwaka 1996 hadi 2003.

Novemba 2018, Burundi iliiomba Mahakama ya Uhalifu wa Kivita kumkamata Buyoya kwa kuhusika na mauaji hayo yaliyosababisha vita nchini humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

error: Content is protected !!