Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mauaji ya mwanachuo KIU: Mtuhumiwa akiri kuhusika
Habari Mchanganyiko

Mauaji ya mwanachuo KIU: Mtuhumiwa akiri kuhusika

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa
Spread the love

ERNEST Joseph (19), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la mauaji ya Anifa Mgaya (21), aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 19 Juni 2019, jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa maeneo ya Madale, Mivumoni jijini humo.

Kamanda Mambosasa amesema, katika mahojiano yake na Jeshi la Polisi, Joseph ambaye kwa jina maarufu anatambulika kama Kibena, alikiri kumchoma kisu marehemu Anifa, tukio lililosababisha kifo cha mwanafunzi huyo.

“Mtuhumiwa katika mahojiano na Jeshi la Polisi amekiri kumchoma kisu kilichosababisha  kifo cha mwanafunzi huyo huku akieleza namna mwanafunzi huyo alivyokuwa amevaa siku hiyo ya tukio kuwa ni tshirt nyeusi,suruali ya Jinsi na Kapelo nyeusi,” amesema Kamanda Mambosasa.

Pia, katika mahojiano hayo Kibena alikiri kumpora Anifa pochi iliyokuwa na simu moja aina ya Tekno, fedha taslimu Sh. 8,000 na vitambulisho mbalimbali ambavyo alivitupa na simu hiyo kuiuza.

“Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili,” amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa amesema tukio hilo lilitokea tarehe 16 Juni 2019 majira ya saa tatu kasorobo maeneo ya Chuo cha Kampala kilichopo Gongo la Mboto. Ambapo mwanafunzi huyo alichomwa na kisu kifuani  upande wa kulia wakati akitoka chuoni na kuporwa pochi iliyokuwa na vitu mbalimbali.

Wakati huo huo, Kamanda Mambosasa amesema tarehe 18 Juni mwaka huu, Jeshi la Polisi limeokota risasi 51 zenye kariba 375 za bunduki za kiraia zinazotumiwa na wawindaji, maeneo ya Ukonga, Gongo la Mboto na Chanika.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum linatoa wito kwa mtu yeyote anayemiliki silaha au risasi kinyume cha sheria wazisalimishe katika kituo chochote cha polisi kilichopo karibu,” amesema Kamanda Mambosasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!