Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mauaji mkesha wa Krismas
Habari za Siasa

Mauaji mkesha wa Krismas

Spread the love

WATU kadhaa wameuawa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria baada ya wanamgambo wa Boko Haram kushambulia vijiji vya Wakristo na kuteketeza Kanisa wakati wa Mkesha wa Krismasi. inaripoti BBC…(endelea).

Vyanzo vya habari katika eneo hilo vinasema, karibu watu wa 11 wameuawa.

Wapiganaji waliingia Pemi katika Jimbo la Borno, kwa kutumia magari na piki piki na kuanza kufyatua risasi holela.

Pemi iko karibu na Chibok ambako wasichana 200 wa shule walitekwa mwaka 2014.

Boko Haram wamefanya mashambulio kadhaa Kaskazini mwa Nigeria ambako wanapigana kupindua serikali ili kubuni taifa la Kiislamu.

Wanavijiji walitorokea msituni na baadhi yao bado hawajulikani waliko.

“Magaidi waliwaua watu saba, kuchoma moto nyumba 10 na kuiba bidhaa za chakula ambazo zilikuwa zigawanyiwe wakaazi wakati wa sherehe ya Krismasi ,”kiongozi wa wanamgambo Abwaku Kabu alisema.

Wasambuliaji walichoma moto kanisa, kumteka mchungaji na kuiba bidhaa za matibabu katika hospitali moja kabla ya kuiteketeza moto.

Mzozo wa Boko Haram ambao umedumu kwa miongo kadhaa, umesababisha mauaji ya watu karibu 36,000 na wengine milioni mbili kufurushwa makwao, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!