Saturday , 20 April 2024
Habari Mchanganyiko

Mauaji mgodini

Spread the love

WATU wanne wameuwawa kwa kushambuliwa kwa mapanga huku mmoja akijeruhiwa mkoani Shinyanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga … (endelea).

Taarifa kutoka kiwanda cha uchenjuaji madini ya dhahabu cha Plant, kilichopo kwenye mgodi mdogo wa Ntambalale katika Kijiji cha Wasolele, Kahama zimeeleza, watu hao wasiojulikana waliwavamia na kuwashambulia.

Akielezea tukio hilo Hamisi Mabubu, mwenyekiti wa mgodi huo amesema, wavamizi hao walifika kwenye kiwanda hicho usiku wa manane jana tarehe 30 Juni 2020 kisha kutekeleza unyama huo.

“Walikuta wafanyakazi watato na ndio walipoanza kuwashambulia huku wakiwashambulia kwa mapanga, walifanikiwa kuiba kaboni. Wanne kati ya hao watano walifariki dunia na mmoja ambaye ni Evvary Mbuya,” amesema akisitiza “chanzo cha uvamizi huo ni tamaa ya kupata mali haraka.”

Joseph Mayala, Diwani wa Kata ya Segese amesema, walipofika kwenye tukio, walikuta miili ya wafanyakazi hao ikiwa imehifadhiwa katika chumba kimoja cha kiwanda hicho.

Na kwamba, walipokuwa kwenye taratibu za kuhamisha miili hiyo, ndio waligundua mmoja kati yao hajafariki “huyu tulimkimbiza hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama,” amesema.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Shinyanga, ACP Joseph Paul amesema, uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na kwamba, watakapopatika awatachkuliwa hatua za kisheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!