Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Matukio kutupa watoto yameongezeka’
Habari za Siasa

‘Matukio kutupa watoto yameongezeka’

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Masauni
Spread the love

BUNGE limeelezwa, katika kipindi cha Januari hadi Juni 2019, kumekuwa na jumla ya matukio 66 ya watoto waliotupwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 4 Septemba 2019 na bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum, Maryam Msabaha ambapo alisema, watoto 43 walikutwa hai na 23 walikutwa wamefariki.

Katika maswali yake mbunge huyo alisema, kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya watoto wachanga kutupwa jalalani, mitaroni na katika mifuko ya Rambo.

Je, nini kauli ya serikali kuhusu matukio haya na je, ni watuhumiwa wangapi walishakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria?

Akijibu swali hilo Masauni alisema, vitendo vya kutupa watoto majalalani, mitaroni na maeneo mengine ni kinyume na sheria za nchi na haki za binadamu.

“Katika matukio hayo watuhumiwa 18 walikamatwa na kufikishwa mahakamani na kesi zao zipo katika hatua mbalimbali,” amesema.

Amesema, kwa mujibu wa kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa  marekebisho mwaka 2002 chini ya kifungu cha 218 na 219.

“Adhabu ya makosa hayo ni kifungo cha maisha na kusema kuwa, serikali inalaani vikali vitendo na itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wale watakaopatikana na hatia,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!