Matenki 3,250 yakuvunia maji yajengwa – MwanaHALISI Online
Tanki la kuvuna maji ya mvua
Tanki la kuvuna maji ya mvua

Matenki 3,250 yakuvunia maji yajengwa

MATENKI 3,250 ya uvunaji maji ya mvua yamejengwa katika maeneo mbalimbali nchini. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu waziri wa Maji, Amos Makalla alipokuwaakijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Amina Makilagi (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua serikali inafikia hatua gani katika utekelezaji wa dhamira ya serikali ya kuhakikisha wananchi wanaondokana na tatizo la ukosefu wa maji.

Akijibu swali hilo, Makalla amesema  hadi sasa zaidi ya matenki 3,250 ya uvunaji maji ya mvua yamejengwa katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika taasisi za shule na vituo vya afya.

Aidha, amesema  wizara imetoa maagizo kwa kila halmashauri kuwa na sheria ndogondogo zenye kuzilazimisha taasisi za serikali na watu binafsi kuweka miundombinu ya uvunaji maji kwenye majengo yao.

Amesema  katika utekelezaji huo, tayari halmashauri 11 zimekwishatunga sheria ndogo ndogo za uvunaji maji ya mvua.

Amesema  halmashauri 18 zinaendelea na taratibu za kukamilisha sheria hizo.

MATENKI 3,250 ya uvunaji maji ya mvua yamejengwa katika maeneo mbalimbali nchini. Anaandika Dany Tibason, Dodoma ... (endelea). Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu waziri wa Maji, Amos Makalla alipokuwaakijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Amina Makilagi (CCM). Mbunge huyo alitaka kujua serikali inafikia hatua gani katika utekelezaji wa dhamira ya serikali ya kuhakikisha wananchi wanaondokana na tatizo la ukosefu wa maji. Akijibu swali hilo, Makalla amesema  hadi sasa zaidi ya matenki 3,250 ya uvunaji maji ya mvua yamejengwa katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika taasisi za shule na vituo vya afya. Aidha, amesema  wizara imetoa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Dany Tibason

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube