Wema Sepetu (mwenye gauni jeusi) akitolewa mahakamani na kupelekwa mahabusu

Masikini Wema! Atupwa mahabusu

Spread the love

WEMA Sepetu, mwigizaji na msanii maarufu wa filamu nchini, amejisalimisha na kutupwa mahabusu baada ya Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam kuagiza kusakwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Maira Kasonde, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo tarehe 11 Juni 2019, alitoa amri ya kumkamata Wema popote alipo baada ya kushindwa kufika mahakamani ili kusikiliza kesi yake inayohusu kuchapisha video chafu mtandaoni.

Msanii huyo amekamatwa leo tarehe 17 Juni 2019, katika Mahakama ya Kisutu baada ya mahakama hiyo kutoa wito wa kukamatwa kwake.

Alipofika mahakamani, Wema alikamatwa na kupandishwa kwenye gari la Magereza na kupelekwa Segerea. Anatarajiwa kufikishwa mahakamani hapo tarehe 24 Juni 2019. Siku hiyo mahakama itaamua kumfutia dhamana ama la!

WEMA Sepetu, mwigizaji na msanii maarufu wa filamu nchini, amejisalimisha na kutupwa mahabusu baada ya Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam kuagiza kusakwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Maira Kasonde, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo tarehe 11 Juni 2019, alitoa amri ya kumkamata Wema popote alipo baada ya kushindwa kufika mahakamani ili kusikiliza kesi yake inayohusu kuchapisha video chafu mtandaoni. Msanii huyo amekamatwa leo tarehe 17 Juni 2019, katika Mahakama ya Kisutu baada ya mahakama hiyo kutoa wito wa kukamatwa kwake. Alipofika mahakamani, Wema alikamatwa na kupandishwa kwenye gari la Magereza na kupelekwa Segerea. Anatarajiwa kufikishwa mahakamani hapo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!