Mashine feki za EFD zaitesa TRA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) inateswa na wafanyabiashara wasio waaminifu na wanaotumia mashine feki za kielektroniki za kukusanyia mapato (EFD). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Charles Kichere, Kamishna Mkuu wa TRA amesema, kwa sasa changamoto hiyo ni kubwa ambapo wafanyabiashara hao wamekuwa wakitoa stakabadhi zenye kiasi kidogo cha fedha walizolipa ili kupunguza kodi.

Akizungumza baada ya kufungua mkutano wa washauri wa kodi jijini Dar es Salaam, Kamishna Kichere changamoto hizo ni miongoni mwa sababu za serikali kukosa mapato.

Amkizungumza katika mkutano huo uliolenga kujadili changamoto ya ukusanyaji kodi, Kamishna Kichere amesema kuna mtandao wa baadhi ya watu wanaotengeneza mashine feki za EFD hutoa risiti za kughushi na kupelekea seriali kukosa mapato.

Kamishna Kichere amesema wamebaini uharifu huo wakati wafanyabiashara wanapofanya mrejesho wa kodi, ndipo TRA ilipobaini risiti feki. Amesema tofauti ya risiti halali na feki ni tofauti ya ukubwa wa maandishi.

Katika hatua nyingine, Kamishna Kichere amesema wako baadhi ya watumishi wanaoshughulika na masuala ya kodi sio waamini kwa kuleta  marejesho  yasiyo sahihi, ambapo hupeleka katika Halmashauri, benki na TRA vitabu vya mahesabu vilivyo ghushiwa.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) inateswa na wafanyabiashara wasio waaminifu na wanaotumia mashine feki za kielektroniki za kukusanyia mapato (EFD). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea). Charles Kichere, Kamishna Mkuu wa TRA amesema, kwa sasa changamoto hiyo ni kubwa ambapo wafanyabiashara hao wamekuwa wakitoa stakabadhi zenye kiasi kidogo cha fedha walizolipa ili kupunguza kodi. Akizungumza baada ya kufungua mkutano wa washauri wa kodi jijini Dar es Salaam, Kamishna Kichere changamoto hizo ni miongoni mwa sababu za serikali kukosa mapato. Amkizungumza katika mkutano huo uliolenga kujadili changamoto ya ukusanyaji kodi, Kamishna Kichere amesema kuna mtandao wa baadhi ya watu wanaotengeneza mashine feki za EFD hutoa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram