Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Masele: Sijawahi kukurupuka
Habari za SiasaTangulizi

Masele: Sijawahi kukurupuka

Spread the love

STEPHEN Masele, Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM) amesema, hajawahi kukurupuka katika kusimamia jambo lolote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kutoka  kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge jijini Dodoma kuhusu tuhuma za utovu wa nidhamu.

“Fuatilia rekodi zangu huko nyuma, chochote ninachokisema ninasimamia haki, ukweli na ninaheshimu viongozi wenzangu,” amesema Masele.

Masele amefika mbele ya kamati hiyo baada ya Job Ndugai, Spika wa Bunge kudai kwamba, mbunge huyo amekuwa akitoa maneno ya hovyo hovyo na hata kugonganisha mihimili miwili ya dola.

Masele ambaye ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), alifika mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na Emmanuel Mwakasaka, Jumatatu ya tarehe 20 Mei 2019 kama alivyoelekezwa na Spika Ndugai.

Mbele ya wanahabari Masele alisema, anatambua miiko ya uongozi kwa kuwa, ameshika nafasi mbalimbali ikiwa ni pamoja na unaibu waziri akisisitiza kuwa, hajawahi kukurupuka katika kufanya uamuzi ama kwenye misimamo yake.

“…ninasimamia haki, ukweli na ninaheshimu viongozi wenzangu , amesema Masele na kuongeza “nimekuwa naibu waziri, natambua miiko ya uongozi.

“Nawahakikishie Watanzania kwamba, kile nilichokuwa nasimamia ni misingi ya haki za binadamu na kufanya hivyo nisitafsiriwe kwamba, ni utovu wa nidhamu.”

Amesema kuwa, amelelewa kwenye familia yenye maadili mema na pia amepitia kwenye umoja wa viajana hivyo hana tabia ya kudharau viongozi wake

“Ninaheshimu sana viongozi wangu, nimelelewa vizuri na wazazi wangu, na chama change pia. Nimetokea umoja wa vijana kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya kitaifa na kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa,” amesema.

Masele hakueleza namna ya mjadala ulivyokuwa mbele ya Kamati ya Maadili, ila ameeleza kuwa na matumaini ya kutendewa haki.

Hata hivyo, Spika Nduga alisema kuwa, baada ya Masele kuhojiwa na kamati hiyo, atahojiwa pia na Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!