
Chris Musando, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Masuala Teknolojia wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka Nchini Kenya (IEBC)
MAUAJI ya Kaimu Mkurugenzi wa Masuala Teknolojia wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka Nchini Kenya (IEBC), yameziibua nchi za Marekani na Uingereza na kuamua kuungana na nchi hiyo kufanya uchunguzi wa kifo cha mtalaam huyo, anaandika Victoria Chance.
Chris Musando ambaye alikuwa msimamizi wa mifumo ya kompyuta ambayo ingesaidia kuzuia wizi wa kura wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwezi huu, aliuawa jumamosi iliyopita nchini humo.
Polisi wameeleza kuwa mwili wa Musando pamoja na mwanamke ambaye hakutambulika ulipatikana jijini Nairobi, eneo la Kikuyu.
Gazeti la Daily Nation limeripoti kuwa Mabalozi wa Marekani nchini Kenya, Robert Godec na Nic Hailey, wa Uingereza wamelaani mauaji hayo na kuongeza kuwa watashiriki katika uchunguzi huo.
More Stories
Kuvunjwa kwa Jiji la Dar giza nene latanda
Ukomo wa urais uheshimiwe
Katiba Mpya: Tuanzie pale alipoishia Jaji Warioba