Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani, Saudi Arabia watibuana
Kimataifa

Marekani, Saudi Arabia watibuana

Spread the love

MARAFIKI wawili, Taifa la Saudi Arabia na Marekani yameingia kwenye mgogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa mtandao wa taarifa, Prince Salman ameishambulia Marekani kwa kusema kuwa, taifa la Saudi Arabia limekuwepo kwa miaka mingi kabla hata taifa la Marekani halijatengenezwa.

Na kwamba, Washington isiibabaishe Saudi Arabia yenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Mwanamfalme wa Saudi Arabia ametoa maneno hayo baada ya Rais Donald Trump kutoa maneno ya kejeli kuhusu utawala wa Saudi Arabia kwamba hauna uhai bila taifa lake.

Mfalme Salman amesema, taifa la Saudi Arabia limekuwepo kwa miaka mingi kabla hata taifa la Marekani kuundwa hivyo Washington isiibabaishe Saudi Arabia yenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Mwanamfalme amesema kuwa, nchi yake haitoilipa Washington kwa ajili ya usalama wake.

Majeshi ya Marekani ni sehemu muhimu ya ulinzi Saudi Arabia kwa muda mrefu sasa.

“Saudi Arabia imekuwepo kabla ya Marekani.Taifa la Saudi Arabia limekuwepo toka mwaka 1744 nikiamini ni miaka 30 kabla ya taifa la Marekani halijatengenezwa”,amesema Salman.

Wiki iliyopita rais Trump alisema kuwa mfalme wa Saudi Arabia hawezi kusalia madarakani kwa zaidi ya wiki mbili bila msaada wa jeshi la Marekani.

Salman nae ametoa jibu kwa tamko hilo na kusema kuwa mtu anapashwa kukubali kuwa kuna wakati rafiki anaweza kuzungumza vitu vizuri na wakati mwingine vitu vibaya.

“Kuna mikwaruzano kama hiyo hata ndani ya familia kwani hakuna rafiki atakaezungumza mambo mazuri kuhusu wewe kwa asilimia mia moja”,aliongeza Salman.

Salman amesisitiza kuwa Saudi Arabia imelipia tayari silaha zote ilizonunua kutoka Marekani na haitotoa hata senti moja kulipia ulinzi wa taifa lake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

error: Content is protected !!