Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani kuwawekea vikwazo washirika wa Korea Kaskazini
Kimataifa

Marekani kuwawekea vikwazo washirika wa Korea Kaskazini

Rex Tillerson, Waziri wa Mashuri ya nchi za kigeni
Spread the love

Marekani inasema itaziwekea vikwazo nchi ambazo zinafanya biashara haramu na Korea Kaskazini, anaandika Hamisi Mguta.

Rex Tillerson, Waziri wa Mashauri ya nchi za kigeni amesema kuwa Ikulu ya White House hivi karibuni itaamua ikiwa itaziwekea vikwazo nchi hizo.

Utawala wa Trump umeamua kuiwekea shinikizo zaidi Korea Kaskazini kufuatia na mpango wake wa nyuklia.

Majaribio ya makombora ya hivi karibuni ya Korea Kaskazini ambayo yamepigwa marufuku na Umoja wa Mataifa yamezua shutuma za kimataifa.

Korea Kaskazini inaaminiwa kupiga hatua katika kuunda makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kufika nchini Marekani.

Onyo la Bwana Tillerson lilitolewa wakati wa kikao cha bunge kuhusu mahusiano ya ya kigeni siku ya Jumanne.

Marekani haina uhusiano wa kibiashara na Korea Kaskazini na imekuwa ikitoa vitisho vya kuyawekea vikwazo mataifa ambayo yanafanya biashara na taifa hilo.

Hata hivyo Bwana Tillerso hakuzitaja moja kwa moja nchi hizo.

Amesema kuwa suala la Korea Kaskazini litazungumziwa na China, mshikika mkubwa wa Korea Kaskazini wakati wa mazungumzo wiki ijayo.

 

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!