DONALD Trump, Rais wa Marekani na Rais Uhuru Kenyetta wa Kenya wamesaini mikataba yenye thamani ya dola za kimarekani 900 milioni, huku sehemu kubwa ya makubaliano ya mikataba hiyo ikiwa ni masuala ya usalama na biashara. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).
Trump na Kenyatta wamesaini mikataba hiyo jana tarehe 27 Agosti, 2018 walipokutana kwa ajili ya kufanya mazungumzo kwenye Ikulu ya ‘White House’ iliyoko mjini Washington nchini Marekani.
Marais hao kwa pamoja walikubaliana kushirikiana katika kupambana na masuala ya usalama na ulinzi hasa kudhibiti vitendo vya kigaidi pamoja na kuboresha ushirikiano katika biashara na uwekezaji.
Katika hatua nyingine, viongozi hao wakuu wa nchi walijadiliana kuhusu masuala ya usafiri, ikiwemo safari za moja kwa moja kutoka Nairobi nchini Kenya hadi New York nchini Marekani zitakazo anza mwezi Oktoba, 2018 na kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba safari hizo zitaimarisha utalii na biashara kwa manufaa ya nchi hizo mbili.
Leave a comment