Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Mapya yaibuka mauaji ya jambazi

SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Taasisi za Kiislam Tanzania ameibuka na kumtetea anayeitwa jambazi aliyeuwawa katika tukio la uvamizi wa ATM, kuwa haukuwa jambazi, anaandika Hamisi Mguta.

Jeshi la Polisi nchini limethibitisha kuuwawa kwa Salum Mohammed Almasi, mmoja wa majambazi aliyekuwa akitekeleza uvamizi wa ATM nje ya jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini, Dar es Salaam.

Baada ya kutoa kwa tukio hilo na polisi kuthibitisha, Sheikh Ponda, amemuandika barua kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kueleza utetezi wake juu ya kijana huyo aliyeuwawa.

Sheikh Ponda amechukua hatua hiyo baada ya kuzungumza na ndugu, jamaa na marafiki wa karibu na mtu huyo ambao wamedhihilisha kuwa Almasi hakuwa na vitendo viovu.

Sheikh Ponda ameuthibitishia mtandao huu kuwa ameandika barua hiyo kwa lengo la kutaka mazingatio katika mustakabali wa taifa.

Barua hiyo ya Sheikh Ponda ilieleza kuwa Mei 14, 2017, Almas alipigwa risasi na polisi hadharani kati ya majira ya saa 3:00-4:00 asubuhi wakati akitembea kwa miguu huko Kurasini.

“Nilipokea taarifa ya kijana Salum Muhamed Almasi aliyeuwawa hadharani kwa kupigwa risasi na polisi majira ya saa 3:00 na 4:00, asubuhi eneo la Kurasini Dar es Salaam akiwa anatembea barabarani kwa miguu.

“Kupitia taarifa ya polisi ni kuwa kijana huyo ni jambazi aliyetaka kupora fedha. Nimekutana na familia ya Marehemu ambaye ni mzaliwa wa Kilwa, familia inamtambua kuwa ni kijana mwema kabisa.

Nimeongea na baadhi ya wakazi wa Kilwa, wao pia wanamtambua kama mtu mwema kwa tabia na anayeshiriki ibada Msikitini ipasavyo,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.

Aidha taarifa hiyo inasema Almasi pia alikuwa Imamu Msaidizi katika moja ya Misikiti huko Kurasini na muda mwingi ni mtu wa masomo.

“Amemaliza elimu ya msingi, kidato cha nne, cha tano, kidato cha sita na mpaka anauwawa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ngazi ya diploma fani ya ICT Network. Mh. Waziri mauwaji kama haya yanazidi kupambamoto Tanzania na yanachafua haiba ya Taifa,” imeeleza barua hiyo.

Hata hivyo wakati akitoa taarifa za ujambazi huo, Kamishna Sirro alinukuliwa akisema: “Inapotokea matukio kama haya wengi wamekuwa wakilinda nduguzao, hauwezi kujua ndugu yako amefanya nini hadi utakapobini ukweli wa jambo.”

Sheikh Ponda ameitaka serikali kutoa tamko la kufafanua mauaji yanayopoteza watu wengi kwa sasa pamoja na yanaendelea kutokea Kibiti, Pwani.

Amesema ikiwa mfumo wa nchi tuliourithi wa Mahakama, Bunge na Serikali una upungufu, basi busara ni kuuboresha na sio kuuhama na kuanzisha mwingine kinyemela.

SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Taasisi za Kiislam Tanzania ameibuka na kumtetea anayeitwa jambazi aliyeuwawa katika tukio la uvamizi wa ATM, kuwa haukuwa jambazi, anaandika Hamisi Mguta. Jeshi la Polisi nchini limethibitisha kuuwawa kwa Salum Mohammed Almasi, mmoja wa majambazi aliyekuwa akitekeleza uvamizi wa ATM nje ya jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini, Dar es Salaam. Baada ya kutoa kwa tukio hilo na polisi kuthibitisha, Sheikh Ponda, amemuandika barua kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kueleza utetezi wake juu ya kijana huyo aliyeuwawa. Sheikh Ponda amechukua hatua hiyo baada ya kuzungumza na ndugu, jamaa na marafiki…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Hamisi Mguta

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube