Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani, akiangalia athari zilizotokana na mapigano ya wakulima na wafugaji
Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani, akiangalia athari zilizotokana na mapigano ya wakulima na wafugaji

Mapigano ya wakulima, wafugaji yamchosha Kikwete

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

MBUNGE wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (CCM) ameitaka serikali kueleza namna ilivyojipanga kupambana na janga la mapigano baina ya wakulima na wafugaji, anaandika Dany Tibason.

Akiuliza swali bungeni leo, mbunge huyo amesema mapigano hayo yamekuwa yakisababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu.

“Je, serikali imejipangaje kupambana na janga hili?” alihoji Kikwete

Akijibu swali hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alikiri kuwepo kwa migogoro hiyo kati ya wakulima na wafugaji katika maeneo kadhaa ndani ya nchi ambayo yamesababisha watanzania kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu.

Amesema katika kukabiliana na hali hiyo serikali kupitia jeshi la polisi inaendelea kushauri mamlaka zinazosimamia matumizi bora ya ardhi kutenga maeneo yatakayotumiwa na wakulima na wafugaji ili kuepusha migogoro hiyo.

Lakini pia Nchemba amesema serikali inatoa elimu kwa wakulima na wafugaji juu ya matumizi bora ya ardhi.

“Aidha jeshi la polisi hufanya doria na misako na kukamata mifugo inayoingia katika mashamba ya wakulima vitendo ambavyo vinasababisha migogoro ya mara kwa mara na kuhatarisha amani,” amesema Nchemba.

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn
MBUNGE wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (CCM) ameitaka serikali kueleza namna ilivyojipanga kupambana na janga la mapigano baina ya wakulima na wafugaji, anaandika Dany Tibason. Akiuliza swali bungeni leo, mbunge huyo amesema mapigano hayo yamekuwa yakisababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu. "Je, serikali imejipangaje kupambana na janga hili?" alihoji Kikwete Akijibu swali hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alikiri kuwepo kwa migogoro hiyo kati ya wakulima na wafugaji katika maeneo kadhaa ndani ya nchi ambayo yamesababisha watanzania kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu. Amesema katika kukabiliana na hali hiyo serikali kupitia…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Dany Tibason

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube