Tuesday , 19 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Maofisa takwimu wafundwa
Habari Mchanganyiko

Maofisa takwimu wafundwa

Washiriki wa mafunzo ya wadadisi na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania bara wakimsikiliza Waziri wa Fesha na Mipango Dr Philip Mpango (hayupo pichani)
Spread the love

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango amewataka viongozi ngazi ya Taifa hadi kijiji kutoa ushirikiano kwa watafiti watakapokuwa wanafanya kazi zao za ukusanyaji wa takwimu na taarifa mbalimbali kutoka katika kaya zilizochanguliwa, anaandika Dany Tibason.

Dr Mpango amesema hayo alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania bara kwa mawaka 2017/18 mkoani Dodoma.

Amesema kuwa viongozi hao kuanzia ngazi ya taifa, mkoa, wilaya,kata na kijiji wanatakiwa kushirikiana na wakusanya tafiti hao watakapokuwa wakifanya kazi zao ili utafiti huo uweze kupata taarifa zilizo sahihi.

Aidha amewataka pia watanzania wote ambao kata zao zimechanguliwa kushiriki,kuhakikisha zinashiriki katika tutafiti huo hivyo wawe tayari kutoa taarifa sahihi za kila mwanakaya mwenye umri kuanzia miaka 5 na kuendelea.

“Nafahamu pamoja na suala la kukusanya takwimu rasmi za serikali ni shirikishi na ni wajibu wa kila mwananchi kutoa taarifa sahihi kwa lengo la kupanga mipango endelevu ya maendeleo”amesema.

Dr Mpango amewataka watafiti hao ambao waliopewa dhamana ya ukusanyaji takwimu za utafiti kwa nchi mzima kufuuata mashariti ya sheria na kanuni za utumishi wa umma.

“Kama mnavyofahamu mnaenda kukusanya takwimu za mapato na matumizi ya kaya binafsi ninawataka mkawe wasiri na kamwe hamtakiwi kuzitoa popote kwa kuwa ni kwa ajili ya matumizi ya kitakwimu tu na sivyo vinginevyo na mkifanya vinginevyo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria ya Takwimu ya mwaka 2015’alisema.

“Nimefurahi kuelezwa kuwa utafiti huu utakusanya takwimu katika kaya binafsi 10,460 kwa Tanzania bara kuanzia Novemba 2017 hadi Novemba 2018 na kwamba kwa kupitia zoezi hili Serikali ya awamu ya tano imetoa ajira ya mwaka mzima kwa vijana wapatao 620 katika maeneo ya vijijini na mijini.”amesema.

Alisema kuwa kutokana na zoezi hilo serikali ingependa kupata takwimu za hali ya umasikini mapema iwezekanavyo hivyo niombe bank ya Dunia iendelee kufanya kazi na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya kuhakikisha juni 2018 inapata matokeo ya awali ya hali ya umaskini hapa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr Albina Chuwa alisema katika zoezi hilo serikali kamwe halitakubali kikundi chochote,chama cha siasa au mtu binafsi kupotosha zoezi hilo la ukusanyaji wa tafiti zitakazokusanywa kwenye kaya husika.

“Naomba nitoe angalizo kwa kikundi,chama chochote,au mtu binafsi asije akijitokeza kuharibu mpango huu wa maendeleo kwa kupotosha maana halisi serikali inavyotaka kujua idadi ya kaya zake”amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Diwani, wananchi wengine 463 wahama Ngorongoro

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Shule zafungwa kutokana na ongezeko la joto

Spread the loveSUDAN Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kuanzia leo Jumatatu,...

Habari Mchanganyiko

Bunge laja na Marathon kuchangia ujenzi wa sekondari

Spread the loveBUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kukusanya fedha...

error: Content is protected !!