Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maneno mazito ya Mbunge wa Chadema baada ya Uchaguzi
Habari za SiasaTangulizi

Maneno mazito ya Mbunge wa Chadema baada ya Uchaguzi

Elia Michael
Spread the love

NENO LA SHUKRANI

Na Elia F Michael

Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu kwa chama wilaya ya Kakonko na Chama Taifa kuniona kama mtu sahihi kugombea nafasi hii ya Ubunge jimbo la Buyungu.

Chama kimefanya jitihada kubwa sana chini ya Mkurugenzi wa chama John Mrema kuanzia mwanzo mpaka Mwisho na zaidi ya yote nimshukuru Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe Freeman Mbowe , Naibu Katibu Mkuu Bara Mhe John Mnyika pamoja na wabunge wote waliofanikiwa kufika Kakonko na Kuzunguka jimbo la Buyungu kuniombea kura hadi kufika kwa wazazi wangu na kuwashukuru kwa kuzaa chema. Hakika jitihada zenu zimezaa matunda na wananchi wametupatia kura nyingi sana.

Pili, nitambue jitihada za Chama rafiki ACT WAZALENDO ambacho kiliamua kuungana na CHADEMA ili kuunganisha nguvu,nawashukuru uongozi wa ACT WAZALENDO Taifa pamoja na Mkoa wa Kigoma na zaidi yote nimshukuru Kiongozi mkuu Kaka yangu Zitto Kabwe kwa kuamua kuniunga mkono na hakika umoja ni nguvu.

Vyama vya upinzani vikiunganisha mipango na kumsemea vizuri mgombea, CCM ni nyepesi sana na ndio maana tumewasinda kwa kukubalika kwa wananchi na tukawashinda kwa kura wao wakaamua kujitangaza chini ya ulinzi mkali wa FFU zaidi ya 400 usiku wa saa kumi huku sisi tukiwa hatuna hata jiwe mkononi. Angalau tumeweza kuwavua nguo hawa kijani kwamba hawakubariki na uwanja wa siasa safi hawauwezi tena. Hongera CHADEMA hongera ACT WAZALENDO.

Tatu, naomba nitoe shukrani zangu kwa TUNDU LISSU, CLA-TZ, COSA-TZ, Mh Pamela Maasay (mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki), Waheshimiwa madiwani wa CHADEMA TZ na wengine wote waliokua nyuma ya harakati hizi. Hakika mmekua sehemu ya ushindi tulioupata!

Ningependa kutoa ushauri wangu kwa makundi yafuwatayo;

1. WANANCHI na WAPIGA KURA.
Kundi la wananchi na wapiga kura ndilo linalopokea huduma kutoka kwa watu wanaokuwa wametangazwa kama washindi wa uchaguzi mbalimbali. Hili kundi lina wajibu mkubwa wa kukumbuka wanasiasa waliwambia nini wakati wa kampeni na hili kundi pia ndilo lina mamlaka ya kushinikiza maamuzi lililofanya yaheshimiwe na tume kwa gharama yoyote.

2. UPINZANI.
Sisi upinzani tuko vizuri sana na aina ya siasa tunazofanya kwenye kampeni tuko sawa kabisa,tunapata matokeo mazuri sana. Japo baadhi ya vyama vya upinzani vinaratibiwa na ccm lakini misimamo na maelezo tunayotoa kwa wananchi ni rahisi kututofautisha. Kudai tutangazwe kwa nguvu ya aina yoyote ile sio wajibu wetu,wananchi wao wana mamlaka hiyo ya kutaka chaguo lao litangazwe. Hivyo basi vyama vya siasa hususani upinzani halisi tunao wajibu mkubwa wa kuendelea kuwaelimisha wananchi wajue umuhimu wa kulinda maamuzi yao kwa gharama yoyote ile.
Njia pekee ya upinzani kulinda maamuzi ya wananchi ni kufungua kesi mahakamani endapo tu vielelezo vinajitosheleza.

3. TUME YA UCHAGUZI.
Tume ya uchaguzi inao wajibu wa kutoa elimu kwa wapiga kura ila haina mamlaka katika kubadili maamuzi ya wananchi. Hivyo acheni kabisa kuwachagulia wananchi juu ya nani ashinde. Najua pia hii yote inatokana na namna ya tume inavyopatikana pengine mwafanya hivyo kumfurahisha mteuzi wenu ila kumbukeni wanaoumia na maamuzi yenu ni wananchi.

4. CCM.
CCM kama chama kingine nyie pia mnao wajibu wa kuteua mgombea mwenye sifa na asiye na madoadoa,unajua viwili vibovu vikishindana lazima kimoja kitapata fulsa ya kuongoza watu. Hivyo basi kumbukeni maamuzi yenu katika hatua za uteuzi yanaweza kutugharimu hata sisi ambao sio wanachama wenu pale ambapo mgombea wenu mlie msimamisha akishinda. Kuweni makini kwenye uteuzi,msiteue mtu kulingana na urefu wa mfuko wake bali uwezo wa bongo yake. Ni muhimu sana. Lakini pia acheni kutumia fulsa ya kusimamia na kuongoza serikali kuingilia vyombo vya dola ili viwasaidie kushinda..Hatua za awali mtafanikiwa japo baadae mtapata shida sana kwa wananchi maana kiwango cha uvumilivu kitapungua.

5. POLISI NA VYOMBO VINGINE VYA DOLA.
Msiiogope CCM mkaisaidia kubaki madarakani,kwenu ninyi hata ccm ikitoka madarakani nyie mtaendelea kutoa huduma yenu kwa wananchi maana nyie ni waajiliwa na watumishi wa UMMA na utumishi wenu hata mkataba wa ajira hausemi kwamba utakoma pale ambapo CCM itaondoka madarakani.

6. MH RAIS.
Kwanza kabisa nikushukuru kwa kutamka tamka kwamba unamtanguliza Mungu kwa kila jambo,lakini pia nikushukuru kwa kuanza kuonana na viongozi wa dini na makundi mengine yanayo kushauri na kukuelekeza kwa ufasaha.

Naomba nikushauri haya.
1. Kipimo cha uongozi bora ni huduma njema kwa wananchi.
2. Ukisemacho wewe na kukiamua kinaweza kuwa sahihi au kisiwe sahihi.
3. Sikiliza wananchi wanasemaje juu yako.
4. Endelea kuwatendea haki wananchi.
5. Kwakua wewe ni mwenyekiti wa CCM na unataka CCM ibaki madarakani, njia pekee ya kuifanya CCM ibaki madarakani japo haiwezekani ni;

1. Kutoa huduma bora kwa wananchi.
2.Kuwatendea haki wananchi ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza.
3.Kuepuka kutumia nguvu ya vyombo vya dola kupingana na maamuzi ya wananchi,hii njia kwa hatua za mwanzoni inaweza kukufurahisha lakini inategemea kiwango cha uvumilivu wa wananchi wenyewe. Ipo siku hawatavumilia nadhani.
4.Kuwapa elimu ya uraia kuliko kuwanyima elimu wananchi. Ukiwapa elimu ya uraia wataelewa kama ulikua sehemu ya waelimishaji lakini ukiwanyima watapewa na wengine NA baadala yake watakuchukia wewe.
5. Acha chama chako kisemwe kwa mabaya na mazuri pia.

Elia F Michael.
Mbunge wa Buyungu nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!