Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Michezo Manara amaliza utata
Michezo

Manara amaliza utata

Haji Manara
Spread the love

MSEMAJI wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa bado yupo sana ndani ya klabu ya Simba na wala hana mpango wa kuondoka katika siku za hivi karibuni kama taarifa za hapo awali zilivyokuwa zinaeleza. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Siku za hivi karibuni Manara alisema kuwa mara anampango wa kuuomba uongozi wa klabu hiyo kupumzika katika nafasi yake ya Mkuu wa kitengo cha Habari ndani ya timu hiyo kutokana na kuteteleka kwa afya yake.

Manara ametoa kauli hiyo leo wakati wa Tamasha la Simba Day lililofanyika kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Jijini Dar es Salaam ambapo aliwaambia mashabiki wa klabu hiyo kuwa wafute mawazo ya yeye kuondoka ndani ya klabu hiyo.

“Niwaambie kitu mashabiki wa Simba, mimi bado nipo nipo sana ndani ya Simba na wala sina mpango wa kuondoka leo wala kesho, naombeni mfute hayo mawazo,” alisema Haji.

Manara ameyaeleza hayo wakati alipomaliza kuwatambulisha wachezaji watakao tumika na klabu hiyo katika msimu ujao wa mashindano huku kukiwa na maingizo mapya saba.

Msemaji huyo ambaye leo alishuka uwanjani hapo na helkopta akiwa sambamba na Msanii wa mziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye alitumbuiza kwenye tamasha hilo.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!