Man Utd, Tottenham vitani leo

Spread the love

LIGI Kuu nchini England inaendelea tena leo tarehe 19 Juni, 2020 kwa mchezo kati ya Tottenham dhidi ya Manchester United ukiwa muendelezo wa Ligi hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea).

Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa kila timu toka kurejea kwa ligi hiyo baada ya kusimama kwa muda wa miezi mitatu kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19.

Pambano hilo litakuwa la kuvutia kutokana na timu hizo kupishana pointi nne tu kwenye msimamo wa Ligi, ambapo Manchester United ina pointi 45, ikiwa ya tano kwenye msimamo, huku Tottenham ikiwa na pointi 41, nakushika nafasi ya sita kwenye msimamo.

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amesema kuwa mshambuliaji wake kinara Harry Kane atarejea kwenye mchezo wa leo baada ya kupona jeraha lake.

Huku kwa upande wa Manchester United inatarajia kupata huduma kutoka kwa kiungo wake Paul Pogba ambaye anarejea leo uwanjani baada ya kutoka majeruhi.

Kwenye mchezo wa raundi ya kwanza Manchester United aliibuka na ushindi wa mabao 2-1, na kuwa ndiyo mchezo wa kwanza Mourinho kupoteza akiwa kama kocha mkuu wa Tottenham.

LIGI Kuu nchini England inaendelea tena leo tarehe 19 Juni, 2020 kwa mchezo kati ya Tottenham dhidi ya Manchester United ukiwa muendelezo wa Ligi hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea). Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa kila timu toka kurejea kwa ligi hiyo baada ya kusimama kwa muda wa miezi mitatu kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19. Pambano hilo litakuwa la kuvutia kutokana na timu hizo kupishana pointi nne tu kwenye msimamo wa Ligi, ambapo Manchester United ina pointi 45, ikiwa ya tano kwenye msimamo, huku Tottenham ikiwa na pointi 41, nakushika nafasi ya sita kwenye…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!