Man Utd, Man City kuanza Ligi mwisho wa wiki hii

Spread the love

KLABU za Manchester United na Manchester City zinatarajia kuanza mbio zake kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza mwishoni wa juma hili baada ya kupumzika kwa wiki moja. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Manchester United atakuwa nyumbani Old Trafford kuwakabili Crystal Palace huku Manchester City itakuwa ugenini dhidi ya Wolves.

Kuchelewa kwa timu hizi kuanza michezo ya ligi kuu nchini humo imetokana na ushiriki wao kwenye michuani ya klabu bingwa kwa upande wa Man City na kombe la Europa kwa Manchester United katika msimu uliomalizika.

Ligi hiyo ilianza 12 Septemba, 2020 kwa kupigwa jumla ya michezo 12, huku ikishuhudiwa bingwa mtetezi Liverpool akianza vyema kutetea ubingwa wake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Leeds United.

Michezo mingine miwili ya Ligi hiyo itaendelea hii leo ambapo Chelsea itakuwa ugenini kuwakabili Brighton huku Sheffield United itakuwa nyumbani wolves.  

KLABU za Manchester United na Manchester City zinatarajia kuanza mbio zake kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza mwishoni wa juma hili baada ya kupumzika kwa wiki moja. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam ... (endelea). Manchester United atakuwa nyumbani Old Trafford kuwakabili Crystal Palace huku Manchester City itakuwa ugenini dhidi ya Wolves. Kuchelewa kwa timu hizi kuanza michezo ya ligi kuu nchini humo imetokana na ushiriki wao kwenye michuani ya klabu bingwa kwa upande wa Man City na kombe la Europa kwa Manchester United katika msimu uliomalizika. Ligi hiyo ilianza 12 Septemba, 2020 kwa kupigwa jumla ya michezo 12, huku ikishuhudiwa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!