Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mambosasa: Tumejiandaa kuwashughulikia ipasavyo Ukonga
Habari za Siasa

Mambosasa: Tumejiandaa kuwashughulikia ipasavyo Ukonga

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa
Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema litawashughulikia kisheria wale wote wenye lengo la kufanya vurugu siku ya uchaguzi mdogo wa Ubunge utakaofanyika tarehe 16 Septemba 2018 katika Jimbo la Ukonga na udiwani katika Kata ya Vingunguti. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo limejiandaa vizuri kusimamia ulinzi na usalama wa raia katika siku hiyo na kuwa kila kituo cha kupiga kura kutakuwa na askari wa vikosi mbalimbali wakifanya doria kila sehemu huku wakiongozwa na askari maalum wa kikosi cha kutuliza ghasia.

“Jeshi halitasita kuchukua hatua za haraka za kisheria kwa mtu yeyote au kikundi cha watu wenye nia ya kufanya vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na kanuni au sheria ya uchaguzi,” amesema.

Mambosasa amesema kuwa wananchi waishio katika jimbo la Ukonga wasiwe na hofu yoyote kwakuwa waliopanga kufanya vurugu watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

“Polisi wataendelea kusimamia hadi utoaji wa matokeo ili asitokee mtu akataka kufanya ndivyo sivyo, kuna watu wamekuwa na tabia wakipiga kura wanang’ang’ania sehemu hizo za kupigia kura kwa lengo la kuja kufany vurugu, kwa namna ambavyo tumejipanga atakayejaribu kufanya atakalo ataishia kwenye vituo vya Polisi,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!