Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mama Samia kumwakilisha JPM uzinduzi wa mkutano wa AALCO
Habari za Siasa

Mama Samia kumwakilisha JPM uzinduzi wa mkutano wa AALCO

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

MAMA Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, anatarajia kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye uzinduzi wa mkutano wa 58 wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (AALCO). Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Hayo amesema Dk. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria leo tarehe 19 Oktoba 2019, wakati akizungumza na wanahabari kuhusu mkutano huo unaoafanyika kwa muda wa siku tano, kuanzia tarehe 21 hadi 25 Oktoba mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Dk. Mahiga amesema Mama Samia ataufungua mkutano huo kwa niaba ya Rais Magufuli, siku ya Jumatatu tarehe 21 Oktoba 2019.

“Mgeni rasmi katika mkutano huu atakuwa Mheshimiwa Mama Samia, kwa niaba ya Rais Magufuli,” amesema Dk. Mahiga.

Dk. Mahiga ameeleza kuwa, washiriki wa mkutano huo ni mawaziri wa shera, wanasheria wakuu pamoja na mabalozi wa nchi 48 kutoka barani Asia na Afrika, ambazo ni mwanachama wa AALCO.

“Washiriki ni mawaziri wa sheria na wanasheria wakuu. Na hapa Tanzania utafunguliwa na Makamu wa Rais, Mama Samia,” amesema Dk. Mahiga.

Dk. Mahiga amesema washiriki wa mkutano huo watajadili masuala mbalimbali kuhusu sheria za kimataifa na changamoto zake.

“Umoja huu ulijikita katika sekta ya sheria. Huu mkutano ambao unafanyika kila mwaka,  Unajishughulisha na masuala ya kisheria katika jumuiya ya kimataifa.  Kuna masuala mengi na changamoto nyingi ambapo nchi moja haiwezi kutatua,” amesema Dk. Mahiga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!