Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mama Kabendera aagwa, kuzikwa Jumatatu Bukoba
Habari za Siasa

Mama Kabendera aagwa, kuzikwa Jumatatu Bukoba

Spread the love

MWILI wa Verdiana Mujwahuzi, Mama wa Mwanahabari Erick Kabendera, leo tarehe 3 Januari 2020, umeagwa katika Kanisa Katoliki la Mt. Francis Xavier, Chang’ombe jijini Dar es Salaam. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Wanaharakati mbalimbali, wanasiasa na wananchi wa kawaida, wameshiriki kuuaga mwili wa Mama Kabendera, aliyefariki dunia tarehe 31 Desemba 2019, katika Hospitali ya Amana.

Miongoni mwa watu walioshiriki kumuaga Mama wa Kabendera ni, Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Onesmo Ole- Ngurumwa, Mratibu Mkuu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC).

Wengine ni Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, John Mnyika Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akitoa salamu za rambirambi kutoka kwa Asasi za Kiraia (AZAKI), Henga amesema Mama Kabendera ameondoka na uchungu wa mwanaye kukaa mahabusu gerezani, na kuahidi kwamba watetezi wa haki za binadamu hawataacha kumtetea Kabendera.

“Tunajua mama anaondoka kwa uchungu juu ya mwanaye na hii inadhihirisha na kauli aliyoitoa kabla ya kufariki. Sisi watetetezi wa haki za binadamu tunahuzunika kwa aliyokutana nayo Erick hata kushindwa kumuaga mama yake.

Tutatoa ahadi tutaendelea kumsaidia kwa msaada wa kisaikolojia na kisheria. Mbele ya mama na madhahabu hii tunaahidi kumsaidia,” ameahizi Henga.

Paul Baregu, Msemaji wa familia ya Kabendera, amesema Mama Mujwahuzi atazikwa siku ya Jumatatu tarehe 6 Januari 2020, nyumbani kwao Bukoba, mkoani Kagera.

Msemaji huyo wa familia amesema kabla ya kifo chake, marehemu alivimba mwili mzima, na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Amana, lakini alifariki dunia kabla majibu ya uchunguzi kutolewa.

“Alisumbuliwa na mwili kuvimba. Alivimba mwili wake wote familia ilimpeka hospitali ya Amana kwa ajili ya uchunguzi. Alifariki dunia kabla ya majibu ya vipimo alivyopimiwa hayajapatikana,” amesema

Akitoa wasifu wa marehemu, Baregu amesema Mama Kabendera alizaliwa mwaka Februari 2 , 1939 mkoani Kagera, ameacha watoto 7 kati ya 8 baada ya mmoja kufariki. Ameacha wajukuu 16 na vitukuu 3.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!