Tuesday , 19 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mama aeleza askari wa wanyamapori walivyombaka
Habari Mchanganyiko

Mama aeleza askari wa wanyamapori walivyombaka

Nondomoli Saile, mmoja wa waathirika wa ubakaji huo
Spread the love

MWANAMKE mmoja mkazi wa Kijiji cha Arash Tarafa ya Loliondo, wilayani Ngorongoro, Arusha, Nondomoli Saile, ambaye ameathirika na vitendo vya ubakaji wakati wa operesheni ondoa wafugaji wilayani humo amesema ipo haja ya waliohusika kukamatwa, anaandika Nasra Abdallah.

Nondomoli amesema haya ikiwa ni siku chache tangu Waziri wa Maliasili Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, kusitisha operesheni hiyo, baada ya kupokea taarifa za ukiukwaji wa sheria za vijiji na uwepo wa minong’ono kwamba operesheni hiyo iliendesha na watendaji wa mamlaka za hifadhi kwa kutekeleza matakwa ya muwekezaji.

Chanzo cha mgogoro huo kimetokana na Mamlaka za Hifadhi, kutaka kumega eneo la kilometa 1,500 la vijiji vilivyopo mpakani mwa hifadhi ya Serengeti ili kupafanya Pori Tengefu, jambo ambalo lilizua hali ya taharuki katika eneo hilo hadi pale Waziri Dk. Kigwangala alipoingilia kati kwa kusitisha operesheni hiyo Oktoba 27.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa wananchi wa vijiji vilivyoathirika na operesheni hiyo, mama huyo amesema wanawake wengi wanaishi na mawazo hadi leo baada ya kufanyiwa vitendo hivyo huku wengi wao wakishindwa kupata tiba kutokana na kuona aibu ya kueleza namna walivyofanyiwa ukatili huo kwa watu.

“Unajua kwa mila na desturi za kimasai ni aibu sana kwa mwanamke kueleza mtu namna ulivyobakwa na hivyo wengi nikiwemo mimi tumeamua kukaa kimya na wala hatujui hao waliotufanyia vitendo hivyo kama wana magonjwa au la na pia huenda hata wengine wamepata mimba.

“Tunachokiomba hapa ni serikali hasa kupitia huyu Waziri wa sasa wa Maliasili alioonesha nia njema ya kulitafutia suluhu mgogoro huu wa Loliondo kuwawajibisha na maaskari waliohusika kutufanyia vitendo hivyo wanawake na kuwafanya kuishi kwa mawazo hadi leo kwa kuwa ni mambo ambayo hayatoki akilini mapema,” ameshauri mama huyo.

Akielezea namna alivyofanyiwa vitendo hivyo vya ukatili, Nondomoli amesema anakumbuka ilikuwa Septemba 19 mwaka huu, asubuhi, askari wa hifadhi walipofika kwenye boma lao na kuwata watoke wote nje ili waweze kuliteketeza na moto.

Hata hivyo mwanamke huyu amesema wakati anajaribu kwenda kuokoa baadhi ya mali, ndipo mmoja wa askari alimkamata na kumbaka na kumsababishia maumivu kwenye maeneo ya mwili wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Diwani, wananchi wengine 463 wahama Ngorongoro

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Shule zafungwa kutokana na ongezeko la joto

Spread the loveSUDAN Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kuanzia leo Jumatatu,...

Habari Mchanganyiko

Bunge laja na Marathon kuchangia ujenzi wa sekondari

Spread the loveBUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kukusanya fedha...

error: Content is protected !!