Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Makontena ya makinikia sasa kuuzwa
Habari Mchanganyiko

Makontena ya makinikia sasa kuuzwa

Spread the love

HATIMAYE Rais John Magufuli ameagiza makontena 277 ya makinikia, yaliyozuiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa zaidi ya miaka miwili yauzwe. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Amesema, baada ya kuuzwa fedha zipelekwe kwenye Kampuni ya Madini ya Twiga, inayomilikiwa na serikali pia Kampuni ya Madini ya Barrick.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 24 Januari 2020, jijini Dar es Salaam, katika hafla ya utiaji saini mkataba wa madini baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Madini ya Barrick.

“Yale Makontena ambayo yako bandarini ambayo tuliyashika sasa mkatafute wabia mkayauze, kwa faida ya Kampuni ya Twiga,” ameagiza Rais Magufuli.

Makontena hayo, yalizuiwa bandarini mwaka 2017, yakiwa njiani kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kuchenjuliwa.

Rais Magufuli alizuia yasisafrishwe baada ya kubaini kuwepo udanganyifu wa viwango vya madini vilivyomo katika makinikia hayo. Kisha aliunda Kamati Maalumu ya Uchunguzi wa Mchanga wa Madini uliomo katika makontena hayo.

Kamati hiyo ya wajumbe wanane iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma, ilibaini kwamba katika makinikia hayo kulikuwa na viwango vingi vya madini hasa ya dhahabu, tofauti na viwango vilivyo vilivyoripotiwa serikalini.

Kufuatia sakata hilo, Rais Magufuli alimfuta kazi Sospeter Muhongo, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, pamoja na kuivunja Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!