Tuesday , 19 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Makonda: Bila Neno la Mungu, Magereza, polisi hawatatosha
Habari MchanganyikoTangulizi

Makonda: Bila Neno la Mungu, Magereza, polisi hawatatosha

Spread the love

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema, Magereza na Polisi hawatatosha iwapo Neno la Mungu halitafanya kazi. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Amesema kuwa, gharama za kujenga uzio mkubwa, mageti zinaweza kuzuiwa ama kupunguzwa iwapo tu watu wataishi na Neno la Mungu.

Makonda ametoa kauli hiyo leo jioni tarehe 26 Desemba 2018 wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Kujenga Umoja wa Viongozi wa Dini uliofanyika kwenye ukumbi wa Mliman City, jijini Dar es Salaam.

“Polisi hawatatosha, magereza hawatatosha endapo tutafanyia kazi ya dini.

“Kama Neno la Mungu litasimama hatutahitaji kuweka mageti, fensi. Gharama hizo zinaweza kuepukwa,” amesema Makonda.

Hata hivyo Makonda ameonesha kutofurahishwa na habari mbaya za viongozi wa dini ambazo huharibu sifa ya kanisa.

Amesema, mengine yanatokea kutokana na watu kutotii viongozi wa dini na kwamba, hofu hiyo imewatoka.

“Hivi Biblia hi ndio ya zamani? Ndio ile ninayoijua? Ifike mahali mtu akiitwa na askofu asijiulize.

“Mchungaji anatembea na house girl (dada wa kazi) tunakaa kimya,”anasema Makonda.

Pia Makonda amewaomba viongozi hao wa dini pamoja na kuwapa watu neno la Mungu, wawaeleze na maisha yao.

“Kama serikali inasema tunaenda vizuri bado na wewe unapaswa kumuonesha,” amesema.

Ameelezea namna Rais John Magufuli alivyoingia na kupindua baadhi ya mambo kwa maslahi ya nchi ikiwa ni pamoja na sekta ya madini.

“Rais Magufuli aliona bora awe mpole pale CCM kabla ya kuingia, maana angeweza kuzuiliwa. Sasa ameingia na amepindua,” amesema.

Ameeeleza kuwa, Rais Magufuli amefanya mengi ambayo watu wasingependa yafanywe kwa kuwa wengi waliishi kwa mazoea.

“Kuna baadhi ya mambo amekuwa akifanya mimi najiulize ningeweza kufanya? Kwa mfanyo haya masuala ya mchanga wa madini na namna mtikisiko wake ulivyokuwa.

“Mnajua kwamba tulikuwa hatuwezi hata kukondroo (kuongoza) ndege zetu wenyewe? Sasa hivi ndio anajenga. Tumwombee,” amesema Makonda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Diwani, wananchi wengine 463 wahama Ngorongoro

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Shule zafungwa kutokana na ongezeko la joto

Spread the loveSUDAN Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kuanzia leo Jumatatu,...

Habari Mchanganyiko

Bunge laja na Marathon kuchangia ujenzi wa sekondari

Spread the loveBUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kukusanya fedha...

error: Content is protected !!