Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Makonda aruhusu daladala kusimamisha wanafunzi, atoa onyo kwa polisi 
Habari Mchanganyiko

Makonda aruhusu daladala kusimamisha wanafunzi, atoa onyo kwa polisi 

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, Paul Makonda, ameziagiza daladala jijini humo, kutowaacha wanafunzi vituoni kwa kigezo cha kubeba abiria kulingana na idadi ya viti ‘level seat’ huku akiwataka kuwasimamisha wasiozidi wanne. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Pia, amepiga marufuku kwa askari wanaozikamata bodabodana na bajaji zinazoingia katikati ya Jiji ‘Posta’ kuacha mara moja ili wajitafutie riziki lasivyo atawachukulia hatua.

Makonda ametoa maagizo hayo leo Jumanne tarehe 2 Juni 2020 katika hafla fupi kupokea shehena ya vifaa tiba vya ujenzi iliyofanyika JKT Mgulani.

Agizo hilo la Makonda kuhusu wanafunzi, amelitoa ikiwa ni siku moja imepita tangu kufunguliwa kwa wanafunzi wa kidato cha sita kuanzia jana Jumatatu ili kujiandaa na mitihani yao ya taifa itakayoanza tarehe 29 Juni au 16 Julai 2020.

Shule zote za msingi na sekondari zilifungwa kuanzia tarehe 17 Machi 2020 ili kuepusha kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa unaotokana na virusi vya corona (COVID-19). Bado shule hizo zimefungwa isipokuwa wa kidato cha sita.

Katika maagizo yake, Makonda amesema, zuio la daladala kubeba abiria ‘level seat’ lilitokana na kuzingatia maagizo ya wizara ya afya ya kuepusha mikusanyiko lakini baada ya wanafunzi hao wa kidato cha sita kufunguliwa, amebaini kusumbuliwa na makonda wa daladala.

Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Mkuu huyo wa mkoa amewaomba watu wa daladala, “kwa sababu ya level seat, nimepita kwa baadhi ya maeneo, nimeona ubaguzi kwa kuwabagua wanafunzi. Wanafunzi wanaopaswa kuingia kwenye daladala wasizuiwe. Kama gari ni level seat, wakisimama wanafunzi wane au watano kuna tatizo gani.”

“Weka level seat zako, simamisha wanafunzi wanne au watano katikati ya gari huku mkizingatia maelekeo ya wizara ya afya na hawa hawawezi kuleta shida,” amesema

Kuhusu bodaboda na bajaji kuingia Posta, Makonda ameema, aliruhusu yeye ili kurahisisha wananchi kufika maeneo hayo katika kipindi hiki cha corona lakini kuna baadhi ya askari kuanzia jana amepata taarifa kwamba wanawakamata.

“Bodaboda pamoja na bajaji ziingie Posta. Kuna mpuuzi mmoja ameanza kuwakamata. Kuna mkuu wa mkoa mmoja wa Dar es Salaam, wale wanaokamata bodaboda tutawachukulia hatua, bado sijatengua kauli yangu,” amesema

Amesema, kumzuia bodaboda anayetafuta riziki yake si sahihi.

Pia, Makonda ameuangiza uongozi wa Kigamboni, kuandaa eneo la ekari 50 zitakazotumika kujenga shule maalum ya vijana kwa masomo ya sayansi.

“Nataka Kigamboni iwe eneo la kuzalisha wana sayansi. Tafuteni eneo tujenge shule na atakayekwenda kwenye hiyo shule ni mwana sayansi kweli. Tunataka tuwe tunazalisha wanasayansi wa kutosha,” amesema Makonda

Amesema, shule hiyo ya kisasa yenye vifaa vyote itapokea wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini iwe kutoka Kolomije, Mtwara au Ukerewe watapewa fursa kigezo ni kuwa mwanasayansi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the loveDEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya Msingi...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the love  DEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya...

error: Content is protected !!