Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Makonda ajitumbukiza kwa wapendanao
Habari Mchanganyiko

Makonda ajitumbukiza kwa wapendanao

Spread the love

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amepanga kuendesha mjadala kuhusu masuala ya uhusiano wa mapenzi. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Amesema, amepanga kufanya hivyo ikiwa ni baada ya kumalizika kwa mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Makonda ametoa kauli hiyo leo tarehe 20 Agosti 2019, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu wanaume wanaowadanganya wanawake kuwaoa na baadaye kuwatelekeza.

“Hatukatazi kuoa idadi ya watu kwa misingi ya imani na matakwa yako, hata kama ukitaka kuoa watu 800 oa lakini usiweke ahadi ambayo mtu anajiandaa kuolewa na wewe, anaanza kupanga mipango ya ndoa, unamvisha pete halafu mwisho wa siku unaingia mitini, huyu umemuharibia kabisa ndoto zake,” amesema.

Amesema, sheria inamlinda mtu huyo na ana haki ya kuchukua hatua za kimahakama na wewe ukawajibika kwa mujibu wa sheria hivyo, wananchi wajipange na mjadala huo, utarudhwa mubashara kupitia vyombo vya habari.

“Na mkisema hili jambo halina maana msiniulize idadi ya watoto wa mtaani mbona wanaongezeka?

“Ukiniambia halina maana, msiniulize suala la vibaka kuongezeka na msiniulize suala la mmomonyoko wa maadili maana yake haya yote ni matokeo ya mahusiano mabovu,” amesema.

https://youtu.be/lmViubkzv80

Aidha, katika mkutano huo Makonda amewataka wataalamu wa Kiswahili kutumia fursa ya kuiendeleza lugha hiyo na kuikuza kufuatia kuanza kutumika katika nchi za SADC.

“Rais kafanikiwa sana kama taifa kwa kukipenyeza Kiswahili kuwa lugha ya nne halali na rasmi katika nchi za SADC,  Kiswahili sasa ni lugha ya 10 Duniani na kwa Afrika ndio namba moja, sasa ni wakati wa kujipanga kukisafirisha kwenda kwenye nchi zingine, walimu na wanaoujua lugha wachangamkie fursa hii,” amesema.

Amesema kuwa Tanzania ni kisiwa cha Amani na ndiomaana mkutano huo umefanyika nchini humo? hivyo una manufaa makubwa kwa sana Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

“Kama ukisikiliza vizuri hotuba ya Rais  Magufuli utafahamu vitu vingi sana hata fursa ya kiswahili nayo hauwezi kuiona?, hauwezi kufanya ya kiuchumi, hauwezi kufanya ya kibiashara hata ya Kiswahili pia hutaki basi olewa na mtu kutoka nchi mojawapo katika nchi za SADC unufaike hilo,”amesema..

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!