Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Makonda achimba mkwara DC, DEC
Habari Mchanganyiko

Makonda achimba mkwara DC, DEC

Spread the love

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametoa siku tano kwa watendaji wa halmashauri zilizoko jijini humo, kuanza utekelezaji wa miradi ya kimkakati iliyokwama. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Makonda ametoa agizo hilo tarehe 22 Machi 2019 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano huo, Makonda amewaonya watendaji hao hasa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Madiwani wa Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam, akisema kwamba Rais John Magufuli hakutoa fedha kwa ajili ya kuweka katika akaunti za benki, bali alitoa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kusaidi wananchi.

 “Rais wetu alitoa pesa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Dar es Salaam, hakutoa pesa ili zikae kwenye akaunti, kwa sababu hiyo tumekaa leo na wakuu wa wilaya na timu nzima ya wakurugenzi wake kupitia kila mradi lengo kuhakikisha kwa nini wamekwama au kutokamilisha mikakati iliyowekwa,” amesema  na kuongeza Makonda;

“Mkuu wa idara yoyote kwenye mkoa kama hajasimamia vizuri miradi maana yake tutasaidia kumsimamia yeye, kuna miradi ya ujenzi katika sekta ya elimu, maji , umeme  na afya. Rais ameshatupatia fedha kujenga hospitali za wilaya na vituo vya afya, kilichobaki ni kila mtendaji atekeleze jukumu lake ili tupate matokeo.”

Halmashauri zilizonyooshewa kidole na Makonda kwa kutotekeleza baadhi ya miradi ni pamoja na Halmashauri ya Ilala, ambapo ametoa siku tatu kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema pamoja na watendaji wake kuhakikisha mradi wa ujenzi wa machinjio ya Vinguguti unaanza kutekelezwa.

“Manispaa ya Ilala wao wamebaki kufanya siasa tu ni kuvutana, kupiga stori na mwisho inaanza kutupa hofu ya kwamba inawezekana kinatafutwa 10% au rushwa badala ya kutimiza kilichotakiwa sasa watendaji wetu wanabaki kuhangaika huku madiwani wetu wakibaki kuvutana,”  amesema na kuongeza Makonda.

“Nimempa Mkurugenzi wa Ilala na Mkuu wake wa Wilaya siku tatu kuhakikisha mkataba wa machinjio ya Vingunguti umesainiwa na Mkandarasi amepatikana na ndani ya siku tano ujenzi uanze, kutokufanya hivyo ni kukubali kwamba wameshindwa kusimamia fedha na miradi ya Serikali.”

Hali kadhalika, Makonda ametoa siku tano kwa Halmashauri ya Kinondoni kuhakikisha mradi wa Coco Beach na masoko yake kuanza kutekelezwa, ikiwa ni pamoja na kumpata mkandarasi wa ujenzi huo.

“Kinondoni tumewapa siku tano mradi wa Coco Beach na masoko yake unatakiwa iwe tayari wameshapata Mkandarasi, kufeli kufanya hivyo ni kwamba hatuwezi kuwa na pesa kwenye akaunti halafu watu wanafanya michakato, vikao wakati wananchi na Serikali wameshakamilisha fedha,” amesema Makonda

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!