Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makonda abanwa mbavu madhabahuni
Habari za Siasa

Makonda abanwa mbavu madhabahuni

Spread the love

KAULI ya Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwamba, hakuwahi kutegemea kuona Mchaga angeweza kutoa msaada kwa walemavu na kwamba, ni jambo la kushangaza, imekera wengi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu …(endelea).

Akiwa kwenye madhabahu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushirika wa Moshi mkoani Kilimanjaro, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally amemwombea msamaha Makonda.

Dk. Bashiru alikuwa akirejea kauli ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Mbunge wa Hai na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Shoo kuhusu kauli za ubaguzi na kiburi.

Makonda alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza wakati wa kuaga mwili wa Dk. Reginald, aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Makonda alisema, “sikuwahi kutegemea hata siku moja kumuona Mchaga anampa pesa mlemavu, Mchaga anatoa pesa kwa mlemavu, ni jambo gumu sana. Mchaga anampa yatima pesa, ni jambo ambalo haliwezi kuelezeka…”

Bila kutaja jina la Makonda, kauli hiyo ilijibiwa vikali na Askofu Dk. Shoo pia Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa.

“Ukiwa na cheo, utajiri au nafasi yoyote Mungu aliyokupa, utumie kwa kunufaisha wengine tuache kiburi, tuache kujitutumua. Viongozi wa huu umri mdogo mdogo, mnafika mnajitutumia kama chatu,  achene,” amesema Askofu Dk. Shoo.

“Tusitengane kwa makabila yetu. Naomba wale wote walioguswa na kauli ile, nitoe msamaha kwa kumuaga Mzee Mengi,… anapotokea kiongozi mwenye mamlaka, wakatoa kauli za kibaguzi, lazima tuungane wote kupinga,” alisema Mbowe kwenye shughuli hiyo.

Dk. Bashiru amesema, alishawahi kumkanya Makonda na kwamba, hii ni mara ya pili, akiongeza “ameanza kubadilika.”

“Nitumie fursa hii kumuombea msamaha kijana wetu Makonda, mimi namfahamu na hii ni mara ya pili nimemsema hadharani , mara ya kwanza nilimsema Simiyu, alikuja ofisini akilia na mara ya pili leo, na ameanza kubadilika,” amesema Bashiru.

Dk. Bashiru amesema, kuna changamoto ya Taifa kutoandaa vyema vijana kuwa viongozi bora, na kwamaba kwa sasa CCM kimejikita katika kuwaandaa vijana ili wawe viongozi bora.

“Kuhusu namna ya kuandaa viongozi wetu kuwa bora, kazi hiyo hatukufanya na hivyo tunazaa matunda ya kutowaandaa viongozi wetu,” amesema Dk. Bashiru.

Akizungumza baada ya Dk. Bashiru kumuombea msamaha, Makonda amemshukuru katibu huyo wa CCM akisema kwamba, kitendo hicho kinaashiria upendo aliokuwa nao kwake.

“Baba Askofu na kaka yangu Mbowe na ndugu zetu, nashukuru sana kwa maelekezo na maonyo yenu, lakini pili nashukuru sana kwa katibu wangu mkuu kusimama na kuomba radhi kwa niaba yangu, huu ni upendo mkubwa sana,” amesema Makonda.

Hata hivyo, Makonda amesema kuwa, kuna tafsiri mbaya pale aliposema kuwa, wachaga hawasaidii watu na kwamba, Dk. Mengi ndiye aliyemshuhudia.

Kwenye madhabahu hayo, Mbowe aliitwa kwenye kupeana mkono na Makonda ikiwa ni ishara ya kuombana msamaha, alifanya hivyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!