Anne Makinda, aliyekua Spika wa Bunge la Tanzania
Anne Makinda, aliyekua Spika wa Bunge la Tanzania

Makinda mwenyekiti mpya wa bodi MHIF

RAIS John Magufuli amemteua Anna Makinda, aliyekuwa Spika wa Mbunge kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), anaandika Faki Sosi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Rais Magufuli amefanya uteuzi huo tangu tarehe 25 Mei mwaka huu. Nafasi hiyo alikuwa nayo Balozi Ali Mchumo.

Sambamba na uteuzi Huo Rais Magufuli amemteua Shabani Lila, aliyekuwa Jaji Kiongozi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa.

Pia Rais Magufuli amemteua Prof. Apollinaria Pereka, aliyekuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)  Morogoro kuwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).

Prof. Pereka amechukua nafasi ya Prof, Frederick Mwanuzi ambaye amestaafu

RAIS John Magufuli amemteua Anna Makinda, aliyekuwa Spika wa Mbunge kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), anaandika Faki Sosi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Rais Magufuli amefanya uteuzi huo tangu tarehe 25 Mei mwaka huu. Nafasi hiyo alikuwa nayo Balozi Ali Mchumo. Sambamba na uteuzi Huo Rais Magufuli amemteua Shabani Lila, aliyekuwa Jaji Kiongozi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa. Pia Rais Magufuli amemteua Prof. Apollinaria Pereka, aliyekuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ¬†Morogoro kuwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Faki Sosi

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube