Tuesday , 19 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Makao Makuu ya Mahakama Dodoma yaiva
Habari Mchanganyiko

Makao Makuu ya Mahakama Dodoma yaiva

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma
Spread the love

JAJI Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma amezindua zoezi la upandaji miti katika kiwanja ambacho itajengwa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania mkoani Dodoma. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Akizindua zoezi la upandaji miti katika kiwanja hicho Jaji mkuu Prof. Juma amesema kuwa miti inazofaida nyingi katika maisha ya mwanadamu hivyo watumishi wa Mahakama Kuu Tanzania hawana budi kuitunza.

Amesema kiwanja hicho ambacho wamepatiwa na Manispaa ya Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa Makao Makuu kitapendeza kama kitakuwa cha mafano katika suala la utunzaji wa mazingira.

Aidha amesema kuwa tafiti zinaonyesha kuwa mtu akipanda heka moja ya miti atakuwa ametoa hewa ya Oxygen kwa watu 18 kwa mwaka mzima.

Awali akisoma taarifa za kiwanja hicho Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Mahakama ya Tanzania, Erasmus Uisso amesema kuwa eneo hilo linaukubwa wa hekta 18.9 sawa na hekari 45.

Amesema katika eneo hilo wanatarajia kujengwa jengo la mahakama kuu, mahakama ya Rufani na masjala kuu na ujenzi unaanza ndani ya mwaka huu.

Amesema kuwa tayari wameshapatiwa hati ya eneo hilo ya miaka 99 na hivi sasa wapo katika mchakato wa kumtafuta mtaalam kwa ajili ya michoro pamoja na gharama za ujenzi.

“Tayari eneo hili tulishalifanyia utafiti wa kisayansi kubaini hali ya miamba pamoja na athari za matetemeko lakini wataalam wa masuala ya jiolojia walituambia kuwa hapa hakuna athari ya matetemeko hivyo tunaweza kuendelea na ujenzi kwani athari ya matetemeko ni kilomita 10 kutoka hapa,” amesema Uisso.

Aidha amesema kuwa pia katika eneo hilo kipo kiwacha chenye mita za mraba 9,000 kwa ajili ya ujenzi majengo ya mahakama kuu kanda ya kati, mahakama ya mkoa, Mahakama ya wilaya pamoja na mahakama ya mwanzo.

Naye Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi aliipongeza Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kupata eneo hilo ambalo litajengwa makao makuu ya moja katia ya mihiri ya taifa.

Prof. Kabudi aliwataka kulitumia vizuri eneo na kujenga mahaka ambayo itakuwa ya mfano na inayoendana na makao makuu ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Polisi waendelea kuwabana wanavunja sheria, operesheni 3D yaendelea

Spread the love  JESHI la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Kimeendelea na...

Habari Mchanganyiko

Jela miaka 25 kwa kukutwa na kilo 107.29 za bangi

Spread the love  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, kanda ya Morogoro imemhukumu miaka...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yamhukumu mwandishi wa habari kifungo cha miezi 6

Spread the loveMahakama ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imemhukumu kifungo cha...

Habari Mchanganyiko

Diwani, wananchi wengine 463 wahama Ngorongoro

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia...

error: Content is protected !!