Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Maji yawakimbiza watumishi Chamwino
Habari Mchanganyiko

Maji yawakimbiza watumishi Chamwino

Spread the love

WATUMISHI wa Zahanati ya Ikowa katika wilaya ya Chamwino wamekimbia kituo chao cha kazi kutokana na ukosefu wa maji. Anaripoti Danson Kaijage, Chamwino … (endelea).

Zahanati hiyo kongwe ambayo inahudumia vijiji vya Ikowa na Makoja, kwa sasa ina mhudumu mmoja ambaye pia anaishi mbali kuliko na huduma ya maji.

Juzi wananchi walimwambia mbunge wa jimbo la Chilonwa, Joel Mwaka kuwa hali katika kijiji chao ni mbaya kwani maji yanapatikana kwa gharama kubwa ambayo huwafanya watumishi kushindwa.

Mwaka alitembelea vijiji cha Mulebe, Ikowa, Makoja na Msalamalo akiongozana na mhandisi wa maji wilaya ya Chamwino, Godfrey Mbabaye na kukutana na vilio vya maji kila kona

Samweli Mtembwele alisema wamehangaika kwa muda mrefu kutafuta maji lakini kila kukicha tatizo linazidi kuwa kubwa na sasa watumishi wa serikali wameanza kukimbia.

“Hali ya maji ni mbaya kijijini kwetu, hadi tunavyozungumza watumishi wa hospitali wameshakimbia wawili na tumebakiwa na mmoja ambaye anaishi mbali kuliko na huduma ya maji hivyo ukienda usiku unakutana na mlinzi tu, tunaomba serikali kuliangalia hilo,” alisema Mtembwele

Tatizo ni kubwa kwa wanawake wanaofika kwenye zahanati hiyo kwa ajili ya kujifungua ambapo hutakiwa kwenda na maji kwa ajili ya huduma na kama hawana hulazimika kwa watumishi kutoa maji majumbani mwao.

Mjumbe wa serikali ya kijiji, Rosemary Mbezi alisema kuna mkandarasi ambaye amechimba kisima katika eneo hilo lakini anauza maji kwa Sh. 200 kwa ndoo yenye ujazo wa lita 20.

Mbezi alisema kwa maisha ya kawaida familia moja inatumia Sh. 2000 kwa siku ili kupata maji ambayo ni sawa na Sh. 60,000 kwa mwezi ikiwa Sh. 720,000 kwa mwaka hivyo wananchi wa kawaida hawawezi kumudu gharama hizo.

Alisema akina mama ndiyo wahanga zaidi kwani hawapati maji lakini pia wanakosa huduma za msingi hospitalini kwa kukosa waganga.

Mwaka aliwataka wananchi kuwa watulivu ili afikishe kilio chao kwa wahusika ambao watalifanyia kazi lakini akasikitishwa na gharama kubwa za maji yaliyochimbwa na mwekezaji kwamba bei yake siyo rafiki kwa mazingira ya kijijini.

Akiwa katika kijiji cha Msamalo, Mbunge huyo alisema wakati wowote kuanzia wiki hii wataalamu wataanza kuchimba kisima katika eneo ambalo walibaini kuna maji ya kutosha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!