Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majengo chakavu Z’bar kufungwa, Dk. Mwinyi atoa maagizo  
Habari za Siasa

Majengo chakavu Z’bar kufungwa, Dk. Mwinyi atoa maagizo  

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi
Spread the love

RAIS wa Zanzibar, Hussein Mwinyi ameagiza Tume ya Uchunguzi wa Majengo ya Kihistoria yaliyoko katika Mji Mkongwe, atakayoiunda, kuwahi kutoa orodha ya majengo chakavu yanayopaswa kufungwa ili kuepusha ajali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, ametoa agizo hilo leo Jumatatu tarehe 28 Desemba 2020, wakati anazungumza na wadau wa Mji Mkongwe, visiwani Zanzibar.

Amesema, hatua hiyo itasaidia kudhibiti maafa kama yaliyotokea katika ajali ya Jumba la Maajabu la Beit Al Ajaib, lililoporomoka na kufukia watu takribani watatu, siku ya Krismasi tarehe 25 Desemba 2020.

Sambamba na ufungwajiwa majengo hayo chakavu, Rais Mwinyi ameagiza tume hiyo atakayoiunda hivi karibuni, kubaini wananchi walioko karibu nayo, ili wahamishwe haraka kabla hawajakumbwa na maafa.

“Ni vizuri sasa hivi tubainishe wazi kwamba majengo gani yanafaa yafungwe mara moja kabla hayajasababisha ajali. Ni vizuri tuhakikishe wakazi gani ambao wako pale wanapaswa kuhamishwa mara moja kabla hayajatokea maafa,” amesema Rais Mwinyi.

Katika kudhibiti maafa hayo, Rais Mwinyi ameagiza tume hiyo itakayoiunda, kutoa mapendekezo ya nini kifanyike katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.

“Mapendekezo kama niliyosema, hayana budi ya kuwa ya muda mfupi, kwanza kwa sasa hivi tufanye nini haraka. Sababu tuna tataizo mkononi , muda wa kati waeleze tufanye nini. Lakini vilevile muda mrefu, sababu bila shaka kuna gharama nyingi zitahitajika,” amesema Rais Mwinyi.

Sambamba na hilo, Rais Mwinyi ameagiza mamlaka zinazoshughulikia Mji Mkongwe, kushirikiana katika ufumbuzi wa tatizo hilo la muda mrefu.

Rais Mwinyi ameahidi serikali yake, itatenga bajeti ya fedha pamoja na kuunda mfuko maalumu wa ujenzi wa Mji Mkongwe na kuomba wadau mbalimbali kutoa mchango wao wa kifedha ili kuuhifadhi mji huo wa kihistoria.

“Lazima tuwe na mfuko maalumu wa ujenzi wa Mji Mkongwe, uhifadhi una gharamna na lazima gharama hizo zibebwe na sasa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ndio wadau wakuu. Kwa hivyo lazima tuanze sisi kama Serikali, tuchangie kwenye mfuko huu maalumu kuhakikisha tunafanya uhifadhi katika Mji Mkongwe,” ameahidi Rais Mwinyi.

Rais Mwinyi amewahakikishia Wazanzibar, Seriklai yake itayafanyia ukarabati majengo yote ya kihistoria ambayo ni chakavu.

“Natumaini tume ya uchunguzi itatueleza nini kifanyike ili tupate ripoti kamili ya mambo gani tunatakiwa kufanya, nataka niwahakikishie Wazanzibar wote. Kwanza kurudisha hadhi ya pale,  lakini vile vile tuna hifadhi majengo mengine ambayo  yako katika hali ambayo si nzuri,” ameahidi Rais Mwinyi.

Kuhusu jengo la Beit Al Ajaib, Rais Mwinyi ameahidi kurudisha hadhi yake kwa kulifanyia ukarabati haraka.

“Tumepotoza nembo ya Zanzibar, hii ndio Icon ya Zanzibar  (Beit  Al Ajaib) hatuwezi kunyamaza kimya, lazima tuchukue juhudi. Kwanza kurudisha hadhi ya pale, lakini tuna hifadhi majengo mengine ambayo  yako katika hali ambayo si nzuri,” amesema Rais Mwinyi.

Aidha, Rais Mwinyi ameagiza tume hiyo kufanya uchunguzi wa sababu zilizopelekea jengo hilo kubomoka.

“Sasa nini ambacho natarajia kutoka kwa tume ya uchunguzi, kwanza kuangalia sababu zipi zilizopelekea mpaka jengo likaanguka, pili kutoa ushauri wa nini sasa kifanyike kama walivyosema wengi. Tatizo siyo Beit Al Ajaib peke yake, tatizo kubwa,” ameagiza Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!