Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa: Tutawahudumia Watanzania wote bila ubaguzi
Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Tutawahudumia Watanzania wote bila ubaguzi

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli itaendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili Watanzania wote zikiwemo za afya, maji, miundombinu na elimu bila ya kujali itikadi zao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Waziri mkuu ameyasema hayo leo tarehe 24 Jumatano, Juni  2020 alipozungumza na wananchi baada ya kutembelea Zahanati ya kijiji cha Nandagala akiwa katika ziara ya kikazi wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, ambapo amewataka wananchi washikamane na Serikali katika kuboresha maendeleo yao.

“Suala la maendeleo halina chama, maendeleo yaliyoletwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni kwa ajili ya wananchi wote, hivyo watu wote tunatakiwa tushikamane kwa pamoja kumshukuru na kumuunga mkono Rais Magufuli kwani shule, hospitali anazojenga zinatumika na watu wote,” amesema

Amesema wananchi wanatakiwa watambue jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Magufuli katika kuboresha huduma za afya.

“Leo nimeshuhudia wagonjwa wakiwa wamelazwa katika zahanati yetu ya Nandagala. Haya ni mafanikio makubwa awali hatukuwa na Zahanati hapa.”

Amesema awali kijiji hicho hakikuwa na Zahanati na wakazi wake waliuguzwa majumbani kwa kushindwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya, ujenzi wa zahanati hiyo umekuwa mkombozi mkubwa hususani kwa wajawazito kwani huduma zote zikiwemo za mama na mtoto zinatolewa hapo.

Vilele, waziri mkuu ametembelea kijiji cha Luchelegwa na amekabidhi gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya cha kata ya Luchelegwa. Gari hilo limetolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ufadhili wa Global Fund.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi gari la kubeba wagonjwa, Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Luchelegwa wilayani humo, Juni 24, 2020. Majaliwa alikuwa katika ziara ya kikazi wilayani humo.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaagiza viongozi wa vijiji vyote ambavyo havina zahanati viongozi wake waanzishe miradi ya ujenzi wa zahanati na watakapokamilisha ujenzi wa maboma Serikali itawapelekea vifaa vya viwandani yakiwemo mabati na misumari.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Luchelegwa, Dt. Codratus Mutabihirwa ameishukuru Serikali kwa kuwapa gari la kubebea wagonjwa kwani awali walikuwa wanapata tabu pale wanapokuwa na mgonjwa anayetakiwa kuhamishiwa hospitali ya wilaya.

Amesema gari hilo litatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa na kwamba watalitunza ikiwa ni pamoja na kuhakikisha linakuwa na mafuta wakati wote. “Tayari tumeshatenga fedha katika bajeti ijayo kwa ajili ya gari hili, hivyo hata matengenezo kinga yatakuwa yanafanyika kwa wakati.”

Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Luchelegwa walitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa kuwapatia gari la kubebea wagonjwa kwa sababu walikuwa wanapata tabu sana hususani kwa wajawazito ambao walikuwa wakihamishiwa hospitali ya wilaya kwani walikuwa wanatumia pikipiki.

Mmoja wa wananchi hao Sauda Kaisi amesema anaishukuru Serikali kwa kuwapelekea gari hilo kwa kuwa Kituo cha Afya cha Luchelegwa hakikuwa na gari la kubebea wagonjwa jambo ambalo lilisababisha baadhi ya ndugu zao kupoteza maisha kwa kushindwa kupata huduma kwa wakati.

Mkazi mwingine wa kijiji hicho Joyce Chimela amesema anamshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa uboreshaji wa huduma mbalimbali kwenye wilaya yao kikiwemo Kituo chao cha Afya cha Luchelegwa ambacho kimepewa gari la kubebea wagonjwa litakalowafikisha kwa wakati hospitali ya wilaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the loveDEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya Msingi...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the love  DEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya...

error: Content is protected !!