Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa aitaka KKKT ikamilishe masharti ya TCU
Habari Mchanganyiko

Majaliwa aitaka KKKT ikamilishe masharti ya TCU

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki inayomiliki Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU), ukamilishe mahitaji ambayo yataiwezesha Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), kukiruhusu chuo hicho kuendelea na udahili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, tarehe 16 Januari 2021, wakati alipokutana Askofu Mteule wa Dayosisi hiyo, Dk. Msafiri Mbilu pamoja na viongozi wengine wapya waliochaguliwa.

Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.

Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya Askofu Mbilu kuiomba Serikali iusaidie uongozi wa Dayosisi hiyo katika kukiwezesha chuo hicho kufunguliwa na kuruhusiwa kufanya udahili.

Mwaka 2018, TCU ilikisitishia chuo hicho kufanya masomo na udahili wa wanafunzi katika ngazi zote za masomo baada ya kukosa vigezo.

“Kamilisheni mahitaji yatakayokifanya chuo chenu kiweze kuendelea kufanya udahili. Taarifa niliyonayo ni kwamba TCU walishakuja kukutana nanyi na kufanya ukaguzi, walitoa mahitaji kadhaa ambayo mnapaswa kuyakamilisha na nimesikia mmeridhia na kazi hiyo inaendelea.”

Mbali na maagizo hayo, pia Majaliwa alitumia fursa hiyo kuwashukuru viongozi wa dini nchini kutokana na mchango mkubwa wanaoendelea kuutoa kwa Taifa.

“Viongozi wa dini ni watu muhimu sana, nchi imetulia na ina amani, hivyo kuwa kimbilio kwa waliokosa amani makwao,” amesema.

Awali, Askofu Mbilu alimweleza Waziri Mkuu kwamba Chuo Kikuu cha SEKOMU kimezuiliwa kufanya udahili kutokana na changamoto mbalimbali za kimfumo wa ndani ya Dayosisi na ndani ya chuo ikiwa ni pamoja na kuwa na viongozi wa kukaimu kwa muda mrefu jambo ambalo kwa sasa tayari limeshapatiwa ufumbuzi.

Alitaja changamoto nyingine ni madeni makubwa yakiwemo ya mishahara ya watumishi, ambapo tayari uongozi umeshaanza kulipa malimbikizo hayo na wameweka mipango ya kumaliza kulipa madeni hayo.

Pia, kiongozi huyo alisema chuo kimeshapata waalimu wa kutosha kwa ajili ya kufundisha wanafunzi mara kitakapofunguliwa.

Askofu Mbilu alisema kabla ya kufungiwa Chuo Kikuu cha SEKOMU, kilikuwa kinatoa elimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu maalumu ya kuwahudumia watu wenye ulemavu katika ngazi ya shahada na shahada ya uzamili, hivyo kimetoa wataalamu wengi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!