Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama yawakaba koo wadhamini wa Lissu 
Habari za SiasaTangulizi

Mahakama yawakaba koo wadhamini wa Lissu 

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeagiza kupekwa mbele ya mahakama, taarifa ya kinachoendelea juu ya matibabu ya mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Lissu anayekabiliwa na mashitaka ya uchochezi, yuko nchini Ubelgiji anakopatiwa matibabu kufuatia kujeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana, tarehe 7 Septemba 2017.

Agizo linalotaka taarifa za kuwapo Lissu nchini Ubelgiji kwa matibabu na hali yake inavyoendelea, limetolewa leo Jumatatu, 25 Machi na Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba.

“Ninaelekeza kuwa siku inayofuata ya kutajwa kwa kesi hii, wadhamini wa Lissu, mje na taarifa hapa Mahakamani kueleza hali ya ugonjwa na kinachoendelea kwa sasa,” alisema Hakimu Simba.

Aliongeza, “siwezi kukuruhusu kujitoa, wakati mshitakiwa hayuko mahakamani.”

Hakimu huyo  alihoji, “nikuruhusu ili iweje? Au unataka kusema, mahakama itajijuwa? Siwezi. Naweza kukuruhusu kujitoa baada ya mshitakiwa kufika mahakamani.”

Kauli ya Simba ilitokana na maelezo ya mdhamini kwa kwanza, Robert Katula, kuwa hana taarifa zozote juu ya mshitakiwa kwa kuwa ameshindwa kupata mawasiliano yake.

Katula alieleza mahakama kuwa tangu kupewa onyo na mahakama la kumtaka kufika mahakamani kila kesi inapotajwa na kueleza maendeleo ya ugonjwa wa Lissu, mshitakiwa huyo ameshindwa kumpa ushirikiano.

“Mheshimiwa Hakimu, kwa kweli sina taarifa zozote zinazomhusu Mheshimiwa Lissu kwa sasa ambazo naweza kuieleza kwa ufasaha mahakama yako tukufu. Hii inatokana na ukweli kuwa sijaweza kupata mawasiliano na kwa kweli, sipati ushirikiano unaostahili kutokana kwa mshitakiwa,” alieleza Katula.

Mbali na Katula, ambaye ni Meneja Mkuu wa Hali Halisi Publishers Limited, mdhamini mwingine wa Lissu, ni Ibrahim Ahmed Kipepe, ambaye alikuwa afisa wa usambazaji wa kampuni hiyo.

Alisema, “hivyo basi, kama utaniruhusu, ninakuomba nijitoe kwenye udhamini huu ili niweze kuendelea na majukumu yangu mengine.”

Kesi hiyo iliyokuja kwa kutajwa leo, imeahirishwa hadi tarehe 25 Aprili mwaka huu.

Mbali na Lissu washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo, ni Simion Mkina, mhariri wa gazeti la MAWIO; Jabir Idrissa, mwandishi wa habari wa gazeti hilo na Ismail Mehboob, mfanyakazi wa kampuni ya uchapishaji wa magazeti ya Jamana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!