Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama yawaachia Bwege na wenzake, Polisi yawang’ang’ania
Habari za SiasaTangulizi

Mahakama yawaachia Bwege na wenzake, Polisi yawang’ang’ania

Spread the love

MAHAKAMA ya Mkoa wa Lindi imewaachia kwa dhamana viongozi waandamizi wa Chama cha Wananchi (CUF), waliokamatwa juzi kwenye kampeni za udiwani Kata ya Kivinje, Kilwa huku Jeshi la Polisi likiendelea kuwashikilia kwa kilichotajwa kuwa wamekosea usajili wa majina yao. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Viongozi hao waliokamatwa tangu juzi jioni tarehe 20 Novemba mwaka huu kwa tuhumiwa ya kutamka maneno ya uchochezi ni pamoja na Suleiman Bungara ‘Bwege,’mbunge wa chama hicho katika jimbo la Kilwa Kusini.

Wengine, ni Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Mbarala Maharagande, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa, Abuu Mjaka na mjumbe wa Kamati Tendaji.

Kwenye mahakama hiyo watuhumiwa hao wamesomewa mashtaka matano yakiwamo ya kutamka meneno ya uchochezi.

Shitaka la kwanza ni la uchochezi linalowakabili watuhumiwa wote watatu kwa kutamka maneno yanayoweza kuhatarisha amani kwenye mkutano wa kampeni za udiwani kwenye Kata ya Kivinje.

La pili ni linamkabili Bungara Mbunge wa Kilwa Kusini la kutamka maneno ya kutishia amani, shitaka la tatu halikusomwa kutokana na mshtakiwa wa kosa hilo Hamidu Bobali Mbunge wa Mchinga hakuwepo mahakamani hapo.

Shitaka la nne linamkabili Maharagande, kwa kutamka maneno ya vitisho kwenye hadhara ambapo shtaka la tano linamkabili Mjaka kutuhumiwa kutoa maneno ya matusi kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo anadaiwa kusema “ukimuona mwana CCM ujue huyo mshipa wake wa akili umeungana na mshipa wa mavi.”

Shauri hilo limeahirishwa mpaka tarehe 3 Desemba, mwaka huu na kwamba watuhimiwa wameachiwa kwa dhamana ya mahakama.

Baada ya kukamilishwa kwa taratibu hizo jeshi la polisi liliendelea kuwashikilia viongozi hao kwa kilichodaiwa kuwa wamekosea kuyasajili majina yao.

Inadaiwa kuwa jeshi hilo limeshindwa kufanya marekebisho hayo leo kwa kile kilichoelezwa kuwa muda wa kazi umeisha hivyo watuhumiwa wataendelea kushikiliwa mpaka kesho asaubuhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!