Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama yaagiza Bulaya, Mdee, Msigwa, Heche kukamatwa
Habari za SiasaTangulizi

Mahakama yaagiza Bulaya, Mdee, Msigwa, Heche kukamatwa

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeamuru kukamatwa kwa wabunge wanne wa Chama cha Demokarasia na Maendeleo (Chadema), kufuatia wabunge hao kushindwa kufika mahakamani. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Uamuzi wa kukamwatwa kwa wabunge hao, imetolewa leo tarehe 15 Novemba 2019, mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa mahakama hiyo, Thomas Simba.

Wabunge wanaowindwa na amri ya kukamatwa, ni mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya; mbunge wa Kawe, Halima James Mdee; Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Akisoma maamuzi ya kukamatwa kwa wabunge hao, Hakimu Simba alisema, amefikia maamuzi hayo, baada ya washitakiwa hao kutofika mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili na bila kutoa taarifa.

Hatua ya Mahakama kuagiza kukamatwa kwa Mdee, Bulaya, Msigwa na Heche,kumekuja miezi tisa  baada ya mahakama hiyo kuwafutia dhamana mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko.

Washitakiwa hao wawili – Mbowe na Matiko – walidaiwa kukiuka masharti ya dhamana waliyopewa na mahakama hiyo. Uamuzi wa kuwafutia dhamana zao, ulitolewa na aliyekuwa Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo,Wilbard Mashauri.

Mbowe na Matiko, walikaa mahabusu kwa zaidi ya miezi mitatu, baada ya kuondolewa kwa dhamana zao. Walirejeshwa uraiani na Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano.

Mbali na hao, wengine waliomo kwenye kesi hiyo, ni Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu (Bara); Salumu Mwalimu na Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar).

Mbowe ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo Na. ** ya mwaka ***. Wote kwa pamoja wanashitakiwa kwa makossa Nane, likiwamo la uchochezi na maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo cha Usafirishaji cha taifa (NIT), Akwilina Akwiline.

Akifuta dhamana ya washtakiwa hao, Hakimu Mashauri alitoa hoja tano kufikia maamuzi yake.

Kwanza, washitakiwa wote wawili (Mbowe na Matiko), walithibitika kuidharau mahakama na kukiuka masharti ya dhamana, waliyopewa katika kesi ya msingi iliyokuwa inawakabili mahakamani hapo.

Hakimu Mashauri alisema, mshitakiwa Na. 1 – Mbowe alishindwa kuithibitishia mahakama pasipo na shaka, kwamba alikuwa mgongwa na alishindwa kurejea nchini kuendelea na kesi yake kwa sababu ya ugonjwa huo.

Pili, licha ya madai ya ugongwa wa Mbowe, na kwamba hakutakiwa kusafiri kwa umbali mrefu kwa ndege, hati yake ya kusafiria, inaonesha kuwa alisafiri umbali mwingine mrefu kwa usafiri huo huo wa ndege, jambo linalothibitisha kuwa alikuwa akiiongopea mahakama na kuidharau kwa makusudi.

“Haiwezi kuingia akilini, kwamba daktari amemzuia mshtakiwa kusafiri kwa ndege kutokana na ugonjwa wake, huku mgonjwa huyo huyo, akitumia usafiri wa ndege kwenda nchini Ubelgiji. Haiwezekaani.”

Tatu, Hakimu Mashauri alisema, mshitakiwa alieleza mahakama kuwa alitakiwa kupumzika. Lakini nyaraka zake za matibabu zinaonesha terehe 8 Novemba, alipata matibabu Dubai kwenye nchi za Falme za Kiarabu (UAE), wakati akijua alitakiwa kuwapo mahakamani.

Nne, ni kwamba mdhamini wa Mbowe, aliiongopea mahakama kuwa mshitakiwa huyo alikwenda nchini Afrika Kusini akiwa mahututi na hakuweza kuongea. Lakini mshitakiwa mwenyewe ameeleza kitu tofauti.

Tano, washtakiwa wote wawili, walishindwa kufika mahakamani tarehe 1 na 8 Novemba 2018 na bila kutoa sababu za msingi. 

Katika maamuzi ya leo, Hakimu Simba alisema kuwa kesi hiyo imechukua muda mrefu na kwamba kukosekana kwa washitakiwa hao, kumeifanya ishindwe kuendelea.

Awali Wakili Mkuu wa Serikali, Faraja Nchimbi, alimuomba Hakimu Simba, kutoka hati ya kukamatwa watuhumiwa hao kwa sababu ya kutohudhiria mahakamani bila kutoa taarifa.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Hakimu Simba aliridhia ombi hilo na kuagiza kukamatwa kwa washitakiwa hao na kufikishwa mbele yake, tarehe 19 Novemba, ili kueleza sababu za kushindwa kufika mahakamani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!