Raia wa Marekani wakichoma bendera ya nchi hiyo katika maandamano ya kumpinga Rais Mteule, Donald Trump

Mahakama Marekani yambeza Trump

RAIA wa Marekani wanaoendesha maandamano na kuchoma bendera ya nchi hiyo, wamemshambulia Donald Trump, rais mteule wa taifa hilo, anaandika Wolfram Mwalongo.

Ni baada ya Trump kusema kwamba, wale wanaochoma bendera ya taifa hilo watakuwa wamepoteza uraia wa taifa hilo au wakubali kifungo cha mwaka mmoja jela.

Trump aliandika hayo kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kwamba “ni marufuku kwa mtu yeyote nchini humu kuchoma bendera ya taifa.”

“Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuchoma bendera ya Marekani, na kama wapo wanaofanya ni lazima wachukuliwe hatua. Labda awe tayari kupoteza uraia wake au mwaka mmoja jela,” ameandika Trump.

Hata hivyo, taarifa hiyo imebezwa na Mahakama Kuu nchini humo ambapo imedai kwamba, hakuna mmarekani anayeweza kupoteza uraia wake kwa kufanya kitendo hicho kwasababu hiyo ni moja ya njia ya uwasilishaji wa hisia za wananchi hasa wasioafiki serikali au uongozi ulioko madarakani.

Vitendo vya uchomaji wa Bendera nchini humo vimeendelea kutokea katika maeneo tofauti kutokana na kumpinga Trump kwa madai kwamba, amekuwa na sera za kibaguzi dhidi ya Wamarekani wageni hasa Waislamu na Waafrika.

Trump anatarajiwa kuapishwa na kuingia Ikulu ya nchi hiyo Januari 20 mwakani.
Wakati huo wafuasi Chama cha Democratic wameendelea kufarijiana kwa kurudiwa kuhesabiwa kura katika majimbo yanayodhaniwa kufanyika udanganyifu dhidi ya mgombea wao Hillary Clinton, analiyeonekana kuongoza kwa kura za jumla zaidi ya milioni mbili dhidi ya Trump mpaka sasa.

RAIA wa Marekani wanaoendesha maandamano na kuchoma bendera ya nchi hiyo, wamemshambulia Donald Trump, rais mteule wa taifa hilo, anaandika Wolfram Mwalongo. Ni baada ya Trump kusema kwamba, wale wanaochoma bendera ya taifa hilo watakuwa wamepoteza uraia wa taifa hilo au wakubali kifungo cha mwaka mmoja jela. Trump aliandika hayo kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kwamba “ni marufuku kwa mtu yeyote nchini humu kuchoma bendera ya taifa.” https://twitter.com/realDonaldTrump/status/803567993036754944 “Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuchoma bendera ya Marekani, na kama wapo wanaofanya ni lazima wachukuliwe hatua. Labda awe tayari kupoteza uraia wake au mwaka mmoja jela,” ameandika Trump. Hata hivyo,…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Masalu Erasto

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube