Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama Dodoma kutoa hukumu ya kesi ya Kubenea
Habari za Siasa

Mahakama Dodoma kutoa hukumu ya kesi ya Kubenea

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo akiwa nje ya Mahakama ya Dodoma
Spread the love

Mahakama ya wilaya ya Dodoma, imepanga kutoa hukumu ya pingamizi lililowekwa na wakili wa mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, katika kesi ya jinai inayomkabili katika mahakama hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Pingamizi hilo linahusu nyongeza ya muda wa siku 60 zilizoombwa na serikali, baada ya muda awali kumalizika.

Katika kesi hiyo, Kubenea anadaiwa kumshambulia kwa mateke, ngumi na makofi, Juliana Shonza, mbunge wa Viti Maalum na sasa ambaye amepata uwaziri.

Upande wa mashitaka umeleta maombi hayo kupitia kifungu cha 225 (4) (C) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20.

Wakili wa utetezi, Isaac Mwaipopo amepinga kuwasilishwa kwa maombi hayo kwa maelezo kuwa yameletwa nje ya muda na kumetumika kifungu kisicho sahihi.

Kwa mujibu wa wakili huyo, kifungu kinachorihusu maombi ya aina hiyo, ni 225 (4) (b).

Amesema maombi ya awali ya nyongeza ya muda yaliwasilishwa mahakamani, tarehe 4 Septemba mwaka jana na hivyo tokea wakati huo, hakuna maombi mengine yoyote yaliyowasilishwa ndani ya muda.

“Mheshimiwa Hakimu, leo ni siku ya 70 tangu serikali kuisha siku 60 za maombi ya serikali. Hivyo basi, maombi haya ya leo, yameletwa mahakamani kinyume na sheria na batili,” ameleza wakili Mwaipopo.

Aliongeza: “Mahakama ni chombo huru na hivyo haipaswi kusumbuliwa na visababu visivyo na msingi. Ninaomba mahakama yako imuachie mshitakiwa na kuifuta kesi hii.”

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi, James Karayemah, amepanga kutoa uamuzi wa pingamizi hilo, tarehe 18 Januari mwaka huu.

Kubenea alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tarehe 5 Julai mwaka jana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Alichokisema Rais Samia baada ya kupokea ripoti ya CAG, TAKUKURU

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake itafanyia kazi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

error: Content is protected !!